Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini,
Prof. James Mdoe akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa wa 15 wa
Kamati ya ICGLR ambayo inahusika na mapambano dhidi ya uvunaji haramu wa madini
katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika unaofanyika jijini Arusha.
Baadhi ya Wajumbe
kutoka Tanzania, Sudan, Sudan Kusini na Rwanda waliohudhuria Mkutano wa
Kimataifa wa 15 wa Kamati ya ICGLR ambayo inahusika na mapambano dhidi ya
uvunaji haramu wa madini katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika
unaofanyika jijini Arusha. Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Madini Tanzania,
Mhandisi Benjamin Mchwampaka na wa pili kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini,
John Nayopa.
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini,
Prof. James Mdoe (katikati,) akiwa na Wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa wa 15 wa
Kamati ya ICGLR ambayo inahusika na mapambano dhidi ya uvunaji haramu wa madini
katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika.
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James
Mdoe, tarehe 25/7/2017, amefungua rasmi Mkutano wa Kimataifa wa 15 wa Kamati ya
ICGLR ambayo inahusika na mapambano dhidi ya uvunaji haramu wa madini katika
nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika.
Mkutano huo unaofanyika jijini Arusha kwa siku tatu umehudhuriwa na nchi
wanachama 12 ambazo ni Tanzania, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda, Zambia, Angola,
Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Sudan na Kenya.
Akifungua mkutano huo, Prof Mdoe alisema kuwa baadhi ya masuala muhimu
yatakayojadiliwa ni pamoja na matumizi ya hati moja ya usafirishaji madini,
kuwianisha sheria za nchi wanachama ili kuwa na uwiano katika kudhibiti
utoroshaji madini, pamoja na urasimishaji wa shughuli za wachimbaji wadogo.
Masuala mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na uongezaji wa ushiriki wa
wanawake katika shughuli za uchimbaji madini, uwazi na uwajibikaji katika
tasnia ya uziduaji (EITI) pamoja na uzuiaji wa watoto katika shughuli za
uchimbaji madini.
Pamoja na kujadili utekelezaji wa malengo mbalimbali ya kamati hiyo na
kupeana uzoefu wa shughuli za udhibiti wa uvunaji wa haramu wa madini katika
nchi hizo, ICGLR itatoka na maazimio yanayopaswa kutekelezwa na nchi wanachama
ili lengo la udhibiti wa uvunaji haramu wa madini lifanikiwe.
0 comments:
Post a Comment