Home » » NSSF YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NA KUPOKEA TUZO KWA UZINGATIAJI WA SHERIA YA SERIKALI MTANDAO, VIWANGO NA MIONGOZO

NSSF YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NA KUPOKEA TUZO KWA UZINGATIAJI WA SHERIA YA SERIKALI MTANDAO, VIWANGO NA MIONGOZO



Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeibuka mshindi wa kwanza na kutunukiwa tuzo kwa
Taasisi zilizofanya vizuri katika uzingatiaji wa Sheria ya Serikali Mtandao, viwango na miongozo kwa taasisi zilizo katika ngazi ya nne ya ukomavu wa TEHAMA Serikalini.

Tuzo hiyo ilitolewa na Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, na kupokelewa na Bw. Donald Mhaiki, Mkurugenzi wa TEHAMA wa NSSF.

Hafla ya utoaji wa tuzo hiyo ilifanyika wakati wa kilele cha Kikao cha 6 cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha International Conference Centre (AICC), jijini Arusha.

Ushindi huo unaonesha jitihada za NSSF katika kuimarisha matumizi ya TEHAMA na kuzingatia kikamilifu sheria, viwango na miongozo ya Serikali Mtandao nchini.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa