Showing posts with label Biashara. Show all posts
Showing posts with label Biashara. Show all posts

NBC Yakutana na Wateja Wake Wakubwa wa Jijini Arusha, Yajadili Fursa, Ufanisi wa Huduma Zake Kwa wateja.

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekutana na wateja wake wakubwa kutoka kampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) wa jijini Arusha ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Benki hiyo pia ilitumia fursa hiyo kujadili na wateja hao namna inavyoweza kuboresha huduma zake kulingana na mahitaji yao.

Katika kufanikisha hilo, jana benki hiyo kupitia timu yake ya Biashara na Uwekezaji (CIB) iliandaa hafla maalum ya chakula cha jioni iliyofanyika jijini humo ikiongozwa na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa benki hiyo Bw, Elvis Ndunguru sambamba na maofisa wengine waandamizi wa benki hiyo kutoka makao makuu na matawi yake ya jijini Arusha.


Akizungumza kwenye hafla hiyo Bw Ndunguru alisema tukio hilo ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuendelea kuwa karibu zaidi na wateja wake kwa nia ya kutambulisha huduma zake mpya ikiwemo huduma ya NBC Connect mahususi kwa kundi hilo la wateja, kupata mrejesho wa huduma hizo kutoka kwa wateja hao sambamba na kutoa fursa kwa wateja kubadilishana fursa za biashara.

“Tukiwa kama muhimili muhimu wa utoaji wa huduma za kifedha nchini, NBC tunatambua umuhimu wa utoaji wa huduma bora kwa wateja na kukuza ushirikiano kati yetu na wateja wetu. Hii inasababishwa na mabadiliko yanayotokana na ubunifu na maendeleo ya kiteknolojia tunayoyafanya kila siku’’

“Hivyo hatua hii ya kukutana na wateja wetu wakubwa inatoa fursa kwetu kuelezea maboresho makubwa tuliyofanya kwenye huduma zetu hivi karibuni sambamba na kutambulisha huduma mpya zilizorahisishwa zaidi kidigitali na zinazoendana na mahitaji ya wateja wetu.’’ Alisema

Aidha, kupitia mpango huo benki hiyo imekuwa ikielezea mikakati yake mipana inayolenga kuwahudumia kwa ufanisi zaidi wateja hao, kuwajengea mitandao ya kibiashara miongoni mwao sambamba na kuwasogezea huduma za kibenki karibu zaidi huku huduma ya NBC Connect ikitajwa kama suluhisho muhimu katika kuwasogezea huduma za kibenki wateja hao wakubwa yakiwemo mashirika na kampuni binafsi, pamoja na taasisi za serikali.

“Tunaamini kuwa msingi wa huduma za kipekee ni kuelewa mahitaji na matakwa ya wateja wetu, matukio kama haya yanatupatia mitazamo au maono yanayotusaidia kuwa wabunifu zaidi na kuboresha uzoefu wa kibenki kwa ujumla.” Aliongeza Bw Ndunguru.

Aidha, Bw Ndunguru alitaja baadhi ya mambo muhimu ambayo benki hiyo imekuwa ikiyazingatia katika kukuza ushirikiano na taasisi za kibiashara hapa nchini kuwa ni pamoja na utoaji wa suluhisho zenye ubunifu katika huduma za kifedha, Ubunifu wa kiteknolojia, Ubia wa kimkakati, Kukuza Ukuaji wa Uchumi pamoja na Uwajibikaji kwa jamii huku kipaumbeke kikiwekwa zaidi kwenye masula ya Elimu, Afya na uhifadhi wa mazingira.

“Hivyo basi NBC tunazialika jumuiya za wafanyabiashara kuangalia fursa na faida za kushirikiana na taasisi hii ya fedha ambayo ina dhamira ya dhati na mafanikio yao, kwa kukuza ushirikiano na kutoa zana zinazohitajika katika ukuaji. NBC inalenga kuwa mshirika mwaminifu anaayetegemewa katika biashara hapa nchini,’’ alibainisha.

Wakizungumzia hatua hiyo baadhi ya wateja wa benki hiyo mkoani Arusha walisema imekuja wakati muafaka hasa katika kipindi hiki ambacho mkoa huo upo kwenye mapinduzi makubwa ya kiuchumi kutokana ustawi mkubwa wa sekta ya utalii ikiwa ni matunda ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kupitia mkakati wake wa Royal Tour.

“Kwa sasa mkoa wa Arusha tupo kwenye kasi kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi yanayochagizwa na ukuaji wa sekta ya utalii, biashara, kilimo na viwanda. Ni habari njema kwetu kuona kwamba benki ya NBC ambayo inatuhudumia wadau wengi kwenye sekta hizi inatuunga mkono kupitia huduma zao za kisasa ikiwemo zile za kidigitali ambazo kiukweli zimekuwa msaada mkubwa hususani kwenye huduma za miamala ya kifedha na makusanyo ya serikali,’’ alisema Bw Abdallah Kiwango kutoka Shirika la hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).


Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw, Elvis Ndunguru (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa ambao ni wateja wa benki hiyo jijini Arusha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo ilifanyika jana jioni jijini Arusha.


Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw, Elvis Ndunguru (kulia) akibadilishana Mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo jijini Arusha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo ilifanyika jana jioni jijini Arusha.





Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw, Elvis Ndunguru (katikati aliesimama) akisalimiana na baadhi ya wateja wa benki hiyo jijini Arusha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo ilifanyika jana jioni jijini Arusha.






Baadhi ya wateja wa benki ya NBC jijini Arusha wakifuatilia hafla hiyo







Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw, Elvis Ndunguru (kulia) sambamba na maofisa wengie wa benki hiyo wakizungumza na wageni waalikwa ambao ni wateja wa benki hiyo jijini Arusha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo ilifanyika jana jioni jijini Arusha.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Dkt. Mpango Azindua Shule ya Sekondari ya Mfano ya Benki ya CRDB, Benki Hiyo Ikitimiza Miaka 30

Arusha 16 Mei 2025 - Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, amezindua rasmi Shule ya Sekondari ya Mfano ya Benki ya CRDB, itayojengwa katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya Benki ya CRDB.

 Shule hiyo ya kisasa ni matokeo ya dhamira ya Benki hiyo ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwekeza kwenye elimu bora kwa watoto wa Kitanzania.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shule hiyo uliofanyika katika seimna ya wanahisa wa Benki ya CRDB kuelekea Mkutano Mkuu, Dkt. Mpango aliipongeza Benki ya CRDB kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kijamii, hususan sekta ya elimu. 
“Nawapongeza kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa sekta binafsi. Mmekuwa mstari wa mbele sio tu kwenye huduma za kifedha bali pia katika kuleta mabadiliko ya kweli kwenye jamii,” alisema Dkt. Mpango huku akiipongeza benki hiyo pia kwa kutimiza miaka 30 tokea kuanzishwa kwake mwaka 1996.

Akizungumza katika semina hiyo ya wanahisa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996, Benki ya CRDB imeendelea kuwa mshirika muhimu wa maendeleo kwa Taifa kwa kutoa huduma za kifedha zenye kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
Shule ya Sekondari ya Mfano ya Benki ya CRDB ina uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 600 na imejengwa kwa viwango vya kisasa ikiwa na madarasa ya kisasa 16, maabara 4, maktaba 1 chumba cha TEHAMA 1, ofisi za walimu na wafanyakazi 11, vyoo 53, miundombinu rafiki kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, pamoja na maeneo rafiki ya michezo. Mradi huu unatarajiwa kugharimu takribani shilingi bilioni 5.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, alisema shule hiyo ni zawadi ya Benki kwa Watanzania katika kuadhimisha miaka 30 ya mafanikio ya benki hiyo. “Tulipojiuliza ni zawadi gani ya kipekee tungeweza kuwapa Watanzania katika kutimiza miaka 30, tulikubaliana kwamba elimu ni urithi wenye nguvu kuliko wote. Shule hii ni ushahidi wa dhamira yetu ya kuwekeza katika kizazi kijacho,” alisema Nsekela.
Nsekela aliongeza kuwa shule hiyo ni sehemu ya mpango mpana wa Benki ya CRDB wa kurudisha kwa jamii katika nyanja za ya elimu, afya, mazingira na uwezeshaji wanawake kupitia CRDB Bank Foundation. “Tunaamini kuwa maendeleo endelevu hayawezi kufikiwa bila uwekezaji wa makusudi katika elimu. Kupitia shule hii, tunaweka msingi wa taifa lenye maarifa, maadili na ushindani wa kimataifa,” alibainisha.
Akitoa salamu zake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb), aliishukuru Benki ya CRDB kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya sekta ya elimu nchini. “Kwa niaba ya Serikali na Wizara ya Elimu, naishukuru sana Benki ya CRDB kwa maono na uamuzi huu wa kujenga shule ya kisasa kwa ajili ya watoto wa Kitanzania. Huu ni mfano hai wa jinsi sekta binafsi inavyoweza kushirikiana na Serikali katika kujenga musatakabali bora kwa watoto na vijana wetu.”
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB Bank Foundation, Martin Warioba, alisema shule hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa Benki ya CRDB kuboresha mazingira ya elimu nchini na kufungua fursa kwa watoto wa Kitanzania. “Mbali na kujenga shule hii ya mfano, tumejipanga pia kuanzisha mpango wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kwa kushirikiana na Wizara ya elimu.”

Uzinduzi wa shule hiyo unachukuliwa kama alama ya mafanikio ya miaka 30 ya Benki ya CRDB, na uthibitisho wa maono yake ya kujenga taifa lenye misingi imara ya elimu, usawa na maendeleo endelevu. “Tunajivunia kuona uwekezaji wetu ukiendelea kuzaa faida zaidi katika jamii,” alisema mmoja ya Wanahisa waliohudhuria semina hiyo.
Wanahisa wa Benki ya CRDB watafanya Mkutano Mkuu wa 30 kesho ambapo ajenda mbalimbali zinatarajiwa kujadiliwa ikiwamo kuidhinisha pendekezo la bodi ya wakurugenzi la gawio la shilingi 65 kwa hisa ikiwa ni ongezeko la asilimia 30 kulinganisha na gawio la shilingi 50 kwa hisa lililotolewa kwa mwaka 2023.





Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

RAIS SAMIA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA WENYEVITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA JIJINI ARUSHA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Viongozi mbalimbali kabla ya kufungua Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 28 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na viongozi wengine wakati wa Wimbo wa Taifa wa Tanzania na ule wa Afrika Mashariki ukiimbwa kabla ya kufungua Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 28 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 28 Agosti, 2024.
Viongozi mbalimbali, Wenyeviti wa Bodi pamoja na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma wakiwa kwenye Kikao Kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 28 Agosti, 2024.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

DKT. SAMIA AWATAKA WAKUU WA TAASISI ZA UMMA KUWA WABUNIFU NA KUTOOGOPA MABADILIKO.


Na. Vero Ignatus

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani amefungua Kikao kazi cha pili cha Wenyeviti wa Bodi ya Watendaji wakuu wa, Taasisi za Umma 2024 ambapo amesema suala la mageuzi ni agenda ngumu lakini mabadiliko yanapokuwepo maendeleo yanatokea uli kulinda rasilimali za wananchi na kutimiza lengo la kuanzishwa kwake

Dkt. Samia ametoa kauli hiyo mapema leo Agosti 28, 2024 wakati akifungua kikaokazi cha Wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa Taasisi za umma kuendelea kufanya mabadiliko ya kiutendaji ndani ya Taasisi hizo ili kuondokana na utegemezi sambamba na kutokuogopa mabadiliko yanapofanyika

Amesema kuwa serikali inaposisitiza mabadiliko, ufanisi, Mashirika yalete faida ni kulinda rasilimali za wananchi ambazo zimewekezwa ndani ya mashirika hayo lakini pia ni kutengeneza lengo la kuundwa kwa mashirika haya kwahiyo mabadiliko hayo yanafanywa kwa lengo tarajiwa na kwa nia njema kabisa ya kujenga uchumi wa nchi

"Mabadiliko haya tunayafamya kwa nia njema ya kujenga nchi yetu katika maamuzi ya Kiutendaji"

Amewataka Wenyeviti hao kujadiliana kwa upana Kauli mbiu hiyo na kuipa nafasi ili Mashirika mengine yaweze kufanya kuendana na mageuzi hayo yenye kuleta mchango mkubwa katika Taasisi hizo kwaajili ya kuweza kuchangia Pato la uchumi wa Taifa

Tunaposisitiza mabadiliko, ufanisi, Mashirika yalete faida ni kulinda rasilimali za wananchi ambazo zimewekezwa ndani ya mashirika hayo lakini pia ni kutengeneza lengo la kuundwa kwa mashirika haya kwahiyo mabadiliko haya tunayafanya kwa nia njema kabisa ya kujenga nchi yetu." Amenukuliwa Rais Samia.

Akitoa Salam kwa niaba ya mkoa,Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda leo agosti 28.2024 amemkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na kumshukuru kwa kutoa shilingi Bil 7 kwaajili ya uapanuzi wa uwanja wa ndege Kisongo Arusha kwani ykarabati huo utaondoa changamoto ya wageni kutoka KIA kuelekea Jijini Arusha

Vile vile Makonda alimkaribisha Dkt Samia kwa kumwambia kwamba mwezi wa 10 mkoa wa Arusha unakwenda kuvunja rekodi ya Guinness iliyowekwa na Ujerumani kwa kua na magari aina ya Land Rover 613 kwa wakati mmoja hii ikiwa ni kutangaza Utalii na vivutio Jijini hapa kwa kuwa kua na aina ya magari hayo elfu moja (1000) kwa wakati mmoja

Aidha,mwezi june 2024 yalifanyika Maonesho ya Karibu Kili Fair 2024 kwa awamu ya tisa likiwa ni jukwaa maalum la kuyaweka pamoja makampuni ya ndani na nje ya nchi yanayohusika na sekta ya Utalii ambapo wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi waliweza kushiriki.

Vile vile ndani ya Kikao kazi hiki nitaomba kwa ridhaa yako Mhe Rais viongozi hawa waweze kukutana na wa fanya biashara mbalimbali wa mkoa huu ambapo siku hiyo ya tar 29 tutachinja ng'ombe zaidi 200 Iwe ni kula na kunywa ili waweze kufahamiana na viongozi hawa kwani wengine wanawaona kwenye luninga na mitandaoni au kwenye Mikutano na hawapati nafasi ya kuwa karibu nao. Alisema Makonda.

"Mahusiano haya yatatuondolea migogoro mingi, malalamiko mengi na hakika tutawaondoa watu waliowateka wafanyabiashara na kuwafanya kama vitega uchumi vyao kwaajili ya kuwapeleka kwa viongozi.Nakushukuru sana Mhe. Rais kwa kutukubalia ombi letu Taasisi za umma wanaokutana kwenye kituo cha kimataifa cha mikutano AICC Jijini Arusha. Alisema Makonda.

Kwa upande wake Msajili wa hazina Bw. Nehemiah Mchechu amesema Ofisi yake imeandaa na kukamilisha mfumo mpya wa ofisi ambao umezingatia mazingira ya sasa ya kiuchumi, kisheria, kibiashara na kijamii ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mchechu ameongeza kuwa “tuna vigezo 10 ambavyo tunavitumia naomba nikiri mbele yako katika Taasisi hizi kuna Taasisi 57 ambazo bado zina changamoto ya kufurahia ule uhuru wa kujiendesha, katika hili tumekuwa na mazungumzo na tumekubaliana kama Taasisi tukae pamoja na kuweka mambo yetu sawa’’

“Kwa kuzingatia mapungufu yalibainishwa katika sheria ya sasa ya msajili wa hazina, uchambuzi wa kina ulifanyika na kwenda kutengeneza sheria mpya ya Mamlaka ya uwekezaji wa Umma, tunamatumaini makubwa sana kwamba sheria hii itakamilika katika bunge hili lakini ndani ya mwaka huu’’ amesema Mchechu na kuongeza:

"Katika utekelezaji wa haya mambo Mhe. Rais tumetekeleza maagizo yako ya kuzingatia mapungufu yaliyopo katika Taasisi za kibiashara na za kimkakati na katika hili, tulifanya uchambuzi wa kina kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, kupitia waraka wetu namba moja wa mwaka 2023 na kuangalia ni Taasisi zipi zipewe uhuru wa kujiendesha’’alisema.












Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

TASWIRA MBALIMBALI YA MAONYESHO YA UTALII YA KARIBU FAIR 2017, KISONGO ARUSHA





Banda la Waandaaji wa Maonyesho ya Utalii ya KARIBU FAIR 2017 (TATO)



Mkurugenzi wa TATO Mhe. Sirili Akko (kushoto) akizungumza na Wakurugenzi wa Orange Media Walter Emanuel na Daniel walivyotembelea Maonyesho ya Utalii ya KARIBU FAIR 2017, Kisongo Jijini Arusha.


Bidhaa (Viatu) vinavyotengenezwa kutoka Magereza ya Karanga, Moshi

Walter Emmanuel kutoka Orange Media alivyotembelea Maonyesho ya Utalii ya KARIBU FAIR 2017, Kisongo Arusha.

Mkurugenzi wa TATO Mhe. Sirili Akko Akizungumza machache na Mkurugenzi Orange Media Co. Ltd Bw. Walter Emmanuel katika Maonyesho ya Utalii ya KARIBU FAIR 2017, Kisongo Jijini Arusha.













































Wakurugenzi wa ORANGE MEDIA Daniel na Walter walivyotembelea Maonyesho ya Utalii ya KARIBU FAIR 2017, Kisongo Jijini Arusha.





























Mkurugenzi wa Orange Media Walter Emmanuel akipozi kwenye kiti kinachotengenezwa na Magereza ya Arusha, alivyotembelea Maonyesho ya Utalii ya KARIBU FAIR 2017, Kisongo Jijini Arusha.









Mkurugenzi Mwenza wa Orange Media Daniel, akipata maelezo kuhusu viatu vinavyotengenezwa na Magereza ya Karanga,Moshi
alivyotembelea Maonyesho ya Utalii ya KARIBU FAIR 2017, Kisongo Jijini Arusha.









Mkurugenzi wa kampuni ya Wendy Vee Bw. Wilson John, inayojishughulisha na kutengeneza Urembo za Taa katika Maonyesho ya Utalii ya KARIBU FAIR 2017, Kisongo Jijini Arusha.

Mkurugenzi wa kampuni ya Wendy Vee Bw. Wilson John akizungumza na mtoto aliyetembelea banda lake


Mkurugenzi wa kampuni ya Wendy Vee Bw. Wilson John akitoa melekezo kwa Wakurugenzi wa Orange Media Walter na Daniel





Mkurugenzi wa kampuni ya Wendy Vee Bw. Wilson John akinogesha banda lake kwa nakshi za Bubbles





















Tukiwa na Mhe. Lazaro Nyalandu katika Banda la Wendy Vee.


















Mkurugenzi wa Wazalendo 25 Blog ,Gadiola Emanuel akijadili jambo na Mkurugenzi wa Orange Media



















































Dk. Elifuraha Laltaika akipiga picha na rafiki yake alivyotembelea Maonyesho ya Utalii ya KARIBU FAIR 2017, Kisongo Jijini Arusha.




Kwa Maelezo zaidi kuhusu Orange Media ,Picha ,Print ,Graphics , Website, Canvas na mengine mengi Piga 0755 643 633 , 0683 113 737 na 0718 036 654.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa