Showing posts with label Afya. Show all posts
Showing posts with label Afya. Show all posts

MAKALLA AIPONGEZA SERIKALI, JKCI YATOA VIPIMO BURE MAGONJWA YA MOYO ARUSHA


Na Pamela Mollel,Arusha 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuimarisha huduma za afya kwa kusogeza huduma za kibingwa za magonjwa ya moyo karibu na wananchi.

 Anasema uanzishwaji wa Kituo cha Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika Hospitali ya Arusha Lutheran Centre (Seliani) utawanufaisha wananchi wa Arusha na mikoa ya jirani, pamoja na watalii na wageni watakaoshiriki michuano ya AFCON 2027.

Mhe Makalla anayasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua zoezi la utoaji wa vipimo na matibabu ya magonjwa ya moyo bure, ambapo jumla ya wananchi takribani 1,200 wamenufaika na huduma hizo, huku Serikali ikiahidi kuwawezesha wananchi wasiokuwa na uwezo wanaohitaji rufaa ili wapate matibabu zaidi katika Taasisi ya Moyo ya JKCI jijini Dar es Salaam. 

Aidha, amewahamasisha wananchi kujiunga na Bima ya Afya kwa Wote ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wakati.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge, amesema katika Kanda ya Kaskazini, magonjwa ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza yameendelea kuonekana kwa kasi, ambapo kupitia programu ya upimaji wa afya, zaidi ya wananchi 3,000 wamejitokeza kupima afya zao. 

Anasema kuwa kati yao, asilimia 9 walibainika kuwa na matatizo ya moyo, huku asilimia 29 wakigundulika kuwa na shinikizo la damu, ugonjwa uliokuwa unaongoza zaidi kwa wananchi wenye umri kati ya miaka 45 hadi 80

Dkt. Kisenge ameongeza kuwa sababu kuu zinazosababisha ongezeko la magonjwa hayo ni kutofanya mazoezi ya mwili, unene uliopitiliza, unywaji wa pombe kupita kiasi, uvutaji wa sigara, pamoja na kutokuzingatia lishe bora, akiwahimiza wananchi kubadili mtindo wa maisha na kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kuepuka madhara makubwa ya kiafya.





 

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mapipa yenye Pombe Haramu aina ya Gongo Yamwagwa Kuzuia Kipindupindu, Jijini Arusha

Mgambo wa jiji Wakimwaga pombe za kienyeji aina ya Gongo zilizokutwa kwenye nyumba za wakazi wa Mtaa wa Matejo jijini  Arusha katika operesheni ya tokomeza kipindupindu iliyofanywa na Halmashauri kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa,kufuatia mazingira machafu na hatarishi ya uandaaji wa pombe hizo,mitaa hiyo ni maarufu kwa uuzaji wa pombe za kienyeji.
Mgambo wa jiji akimwaga pombe za kienyeji aina ya Gongo zilizokutwa kwenye nyumba za wakazi wa Mtaa wa Matejo jijini  Arusha katika operesheni ya tokomeza kipindupindu iliyofanywa na Halmashauri kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa,kufuatia mazingira machafu na hatarishi ya uandaaji wa pombe hizo,mitaa hiyo ni maarufu kwa uuzaji wa pombe za kienyeji.
Mgambo wa jiji akimwaga pombe za kienyeji aina ya Gongo zilizokutwa kwenye nyumba za wakazi wa Mtaa wa Matejo jijini  Arusha katika operesheni ya tokomeza kipindupindu iliyofanywa na Halmashauri kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa,kufuatia mazingira machafu na hatarishi ya uandaaji wa pombe hizo,mitaa hiyo ni maarufu kwa uuzaji wa pombe za kienyeji. Picha na Ferdinand Shayo

Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog,Arusha.

Wananchi wa Mtaa wa Matejo uliopo jijini Arusha wameiomba serikali iwapatie mikopo ili waweze kufanya shughuli mbadala za kujiingizia kipato badala kujishughulisha na uuzaji wa pombe haramu ambazo zinadaiwa kuwa sababu mojawapo ya kuenea kwa ugonjwa wa kipindu pindu kutokana na mazingira machafu na hatarishi ya uandaaji wake.

Wananchi hao wakizungumza katika operesheni  ya tokomeza kipindupindu iliyoendeshwa na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ,kwa kushirikiana na Halmashauri na kamati ya Ulinzi na usalama wameteketeza mitambo ya kupikia pombe hizo aina ya piwa,dadi na chang`aa  ambazo pia huathiri afya za watu.

Ester Stephano Shaka  ambaye ni Muuzaji wa pombe hizo na Wilfred Lyakimu na walisema kuwa maisha yao yanategemea biashara ya pombe za kienyeji ambazo huwasaidia kusomesha watoto na kupata mahitaji ya nyumbani hivyo ameiomba serikali iwapatie mikopo ili waweze kufanya biashara mbadala badala ya kutumia nguvu kutokomeza biashara hiyo.

“Tunategemea shughuli ya kupika na kuuza pombe za kienyeji kuendesha maisha yetu ,serikali haiwezi kuwaajiri watu wote tunaiomba serikali itutafutie shughuli mbadala kwani hapa ndio tunapata chakula na mahitaji muhimu “ Alisema Wilfred

Mkazi wa Matejo Jovan George alisema kuwa kutokana na tatizo la ajira limewapelekea watu wengi kujiingiza katika biashara hiyo na matumizi ya pombe hivyo ameitaka serikali kutafuta njia mbadala .

Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira jiji la Arusha  ,James Lobikoki alisema kuwa uteketezaji wa pombe haramu ni moja kati ya jitihada wanazozifanya katika  utekelezaji wa operesheni tokomeza kwani kutokana na mazingira machafu ya uandaaji wa pombe hizo kwani zoezi hilo ni endelevu.

Alisema Ugonjwa wa kipindupindu umeenea katika maeneo mengi nchini tayari wananchi wameanza kuchukua tahadhari ya kuweka mazingira safi licha ya baadhi ya maeneo kukithiri  kwa uchafu hivyo kukwamisha jitihada za kutokomeza ugonjwa huo.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

JK KATIKA HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI ILIYOANDALIWA NA NSSF JIJINI ARUSHA


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ndg. Aboubakar Rajab wakati wakiingia Ukumbiti tayari kwa kushiriki chakula cha jioni na Wadau mbali mbali wa NSSF wanaohudhulia Mkutano wa Nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSSF.Tafrija hiyo imefanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Mount Meru,Jijini Arusha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi tuzo kwa Makampuni na Mashirika mbali mbali ambayo idadi kubwa ya wafanyakazi wake ni wanachama NSSF,wakati wa tafrija ya Chakula cha jioni iliyofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru,Jijini Arusha. 
Mmoja wa wageni waalikwa katika Mkutano wa Nne wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya NPF-NSS,akiwasalimia wadau.
Seheu ya Wakurugeni wa Mifuki ya hifadhi za Jamii wakiwa kwenye tafrija hiyo.
Wadau Mbali mbali.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Lady Jay Dee akitoa burudani kwenye hafla hiyo.
Mkongwe wa Muziki wa Dansi nchini,Mzee King Kikii a.k.a Mzee wa Kitambaa cheupe akizikonga vilivyo nyoyo za Mashabiki wake wakati wa hafla hiyo.

Kitambaa cheupe juu.

Rais Kikwete pia alijumuika na Wadau wa NSSF kuyarudi mangoma ya Kitambaa cheupe.
Wadau.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

HOSPITALI YA KALOLENI YATEMBELEWA NA WAJUMBE WA MKUTANO WA WANAWAKE NA VIJANA WA KIKRISTO DUNIANI


 Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani walipofanya ziara katika kituo cha afya cha Kaloleni jijini arusha kujionea hali ya huduma kwa akina mama wajawazito na wasichana wenye ujauzito.
 Bi Severa joseph akitoa maelezo ya aina ya dawa zinazotumika kwa akina mama wajawazito katika kituo cha afya Kaloleni cha jijini arusha kwa baadhi ya washiriki wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani.
Dr Anna Kimaro mganga wa zamu wa kituo cha afya Kaloleni aliyebeba faili kwapani akiwa na wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani YWCA walipo tembelea katika kituo hicho jijini arusha.
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani walipofanya ziara katika kituo cha afya cha Kaloleni jijini arusha kujionea hali ya huduma kwa akina mama wajawazito na wasichana wenye ujauzito.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani walipofanya ziara katika kituo cha afya cha Kaloleni jijini arusha wakipata maelezo ya kina kutoka kwa moja ya wafanyakazi wa kituo hicho.


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa