Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo katika kikao kazi na timu itayotekeleza mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya tatu ofisini kwake jijini Arusha leo.
Wajumbe wa kikao kutoka
kushoto ni Rama Shankar na Abas Kitola wa Angelique Int. Ltd, Eng.
Donasian Shamba wa TANESCO Arusha na Eng. Gaspar Msigwa ambaye ni
Meneja TANESCO Arusha
Sehemu
ya wajumbe wa kikao hicho kutoka kushoto ni Chuwa African wa TANESCO
Arusha, Wilson Chilewa na Kurwa Nelson wa NIPO Group Ltd.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo leo amekutana na timu itayotekeleza mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya tatu katika kikao kazi kilichofanyika ofisini kwake jijini Arusha.
Mhe Gambo ameshauri wakandarasi wanaotekeleza mradi huo kuwa makini katika masuala ya ajira hasa zile za vibarua kwani mara nyingi zinaleta malalamiko kwa serikali, hivyo amewataka kuwa makini katika kufuata taratibu za ajira za vibarua.
Mkuu wa Mkoa huyo pia amemshauri mkandarasi kua makini na 'sub contractors' wanaowapa kazi kazi mara nyingi wamekua wanafanya utapeli wa kuchangisha wananchi hali inayopelekea kuichafua serikali hususani Shirika la Umeme Tanesco.
"Mara nyingi watu mnaowapa kazi wanakua wanafanya vitendo vya kitapeli kwa wananchi, kwani wanakua wanapita na kuchangisha wananchi michango ambayo kimsingi ni makosa mfano wanaweza kuwaambia wananchi wachange hela ya nguzo ama kuchimba mashimo ya nguzo,nendeni mkakemee vitendo hivyo" alisema Mhe. Gambo.
Mradi huo unategemea kuanza mapema mwezi Agosti na utatekelezwa katika maeneo mbalimbali mkoani Arusha ambao una changamoto kubwa ya umeme.

0 comments:
Post a Comment