Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu
wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu , Seperatus Fella,
akizungumza na wadau kutoka taasisi zinazojihusisha na kupambana na
biashara hiyo waliokutana katika jijini Dar es Salaam leo, ili kujadili
mikakati ya kutokomeza biashaara hiyo nchini. Kikao hicho kimefanyika
katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Afisa
uchunguzi Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya
Usafirishaji Binadamu, Ahmed Mwendadi, akifafanua jambo kwa wadau kutoka
Taasisi zinazopambana na biashara hiyo waliokutana jijini Dar es
Salaam, ili kujadili mikakati ya kutokomeza biashaara hiyo. Kikao hicho
kimefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa ANPPCAN Tanzania, Wilbert Muchunguzi, akieleza jambo juu ya
shughuli wanazofanya katika kupambana na Biashara Haramu ya Kuzuia
Usafirishaji Binadamu nchini. Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Kuzuia
Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Seperatus Fella. Kikao hicho
kimefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi
wa kituo cha C-sema, Michael Kehongoh, akieleza jambo juu ya shughuli
wanazofanya katika kituo hicho kuunga mkono harakati za kupambana na
Biashara Haramu ya Kuzuia Usafirishaji Binadamu nchini. Kushoto ni
Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu , Seperatus
Fella. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments:
Post a Comment