ZAIDI ya vijana 6,000 wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha,
wamenufaika na elimu ya malezi na maadili mema ambayo itawawezesha wawe
na utu na kuboresha familia zao
Hayo yalisemwa na Askofu Mkuu wa jimbo hilo, Mhashamu Josephat Lebulu
(pichani) alipozungumza katika maadhimisho ya sherehe za upadrisho wa
mashemasi watatu, zilizofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Burka,
juzi.
Askofu Lebulu alisema kuwa jimbo hilo linapenda kuwaandaa viongozi
wakiwa wadogo kupitia shule za pekee za seminari za jimbo hilo ikiwemo
ya Usa River, ambayo ni kwa ajili ya wavulana pamoja na ya seminari
iliyopo Kisongo ambayo ni ya kuwaandaa wasichana waweze kukua katika
maadili mema.
Alisema mmomonyoko wa maadili, unazidi kuongezeka katika jamii
kutokana na wazazi kushindwa kusimamia malezi ya watoto na kwamba wao
kama kanisa wamejiwekea utaratibu wa kuelimisha vijana ambao wamemaliza
darasa la saba ili kuwajengea maadili ambayo yatawajenga katika utu.
Mkurugenzi wa Miito katika jimbo hilo, Padri Fulgence Mallya alisema
kuwa kupatikana kwa mapadri hao ni neema, kwani awali ilikuwa changamoto
na kwamba wataweza kusaidia Kanisa Katoliki kufikia watu wengi kupatiwa
huduma.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment