Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Baraza la Madiwani Jiji la Arusha linezindua kanuni mpya zitakazoongoza baraza hilo kwa mujibu wa sheria.
Aidha
baraza hilo linachagua Naibu Meya ili aweze kuongoza baraza hilo kwa
kipindi kingine cha mwaka mmoja huku madiwani wawili wanawania nafasi
hiyo kuwa ni Abdulrasul Tojo Diwani wa Kata ya Mjini Kati huku aliyekuwa
Naibu Meya wa Jiji hilo, Viola Lendikoki akitetea nafasi yake.
Akizindua
kanuni hizo mpya, Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro alisema kanuni
hizo ndizo zitakazoongoza madiwani hao kuendesha vikao vyao vya baraza
hilo la madiwani pia alisisitiza madiwani hao kuzingatia kanuni hizo
zilizosomwa na mwanasheria wa Jiji la Arusha.
Baada
ya uzinduzi wa sheria hizo, wenyeviti wa kamati mbalimbali za kudumu
waliwasilisha taarifa za kamati zao za ikiwemo Kamati ya Uchumi, Elimu
na Afya, Kamati ya Mipango miji, Mazingira na Ujenzi sanjari na Kamati
ya Kudhibiti Ukimwi.
Akiwasilisha
taarifa ya ripoti ya kamati ya Uchumi, Afya na Elimu na Diwani wa Kata
ya Ngarenaro, Isaya Doita alisema wamehamasisha kaya 2,157 kujiunga na
Tika ikiwemo ununuzi wa madawati 1,800 katika shule za msingi
Huku
Mwenyekiti wa Kamati ya Mipangomiji Ally Bananga akiwasilisha ripoti
yake alisema ufinyu wa bajeti kwa mwaka wa Fedha 2016/17 umepelekea
baadhi ya maeneo kushindwa kuboresha mazingira pia mgao wa maji AUWSA
unafanya bustani za mizunguuko kutokuwa kijani cha kuvutia ikiwemo
kuangalia uwezekano wa kuchimba visima kwenye maeneo mbalimbali ya
Jiji.
Awali
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia aliwapongeza madiwani
hao kufikisha mwaka mmoja ikiwemo kutekeleza na kusimamia shughuli
mbalimbali za Jiji la Arusha sanjari na kushirikiana na wataalam wa Jiji
katika kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unavuka leo.
Baraza
hilo la madiwani limemaliza mwaka mmoja jana huku wabunge wa Viti
maalum Mkoa wa Arusha, Catherine Magige kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM)
na Joyce Mukya wakihudhuria baraza hilo sambamba na makatibu wa vyama
mbalimbali vya siasa pamoja na wanachi wa Jiji la Arusha.
0 comments:
Post a Comment