MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaondolea hofu watumiaji wa
mitandao ya simu, wanaotaka kutumia huduma ya laini moja kwa mitandao
yote, kuwa hatawakosa huduma zinazotolewa na makampuni ya simu.
Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Tehama wa mamlaka, Nehemia
Mwenisongole, alisema hayo Jijini Arusha jana wakati akizungumza na
waandishi wa habari. Alisema huduma hiyo itakuwa ya hiari kwa watumiaji
wa mitandao ya simu na itawasaidia kuondokana na kumiliki utitiri wa
laini nyingi za simu na kutumia laini moja, iliyobeba mitandao yote ya
simu ambayo atahitaji kutumia.
“Ukiamua kuhamia kwenye mfumo huu wa kuunganishwa kutumia namba moja,
hakutakuwepo na madhara ya kuanza kuwaza kuwa wapo watu ambao
nitawapoteza nikiingia huko,’’ alisema. Alisema kuingia kwenye mfumo
huo, kutasaidia kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mtandao mahali
mtumiaji atakapokuwa na kumsaidia kutumia mtandao mwingine.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment