Na Woinde Shizza,Arusha
Mgogoro wa ardhi katika tarafa za loliondo na sala zilizopo wilayani
ngongoro umeendelea kuchukuwa sura mpya kutokana na serekali
kusimamia hoja zake za kutaka kuwaondoa wafugaji kutoka katika maeneo
ya vijiji vyao.
Pia Mashirika ya kiraia yanayojihusisha na utetezi wa haki za binadamu
na haki za ardhi wamelalamikia kitendo cha serekali kusitisha mpango
ulinzishwa hivi karibuni wa kupima vijiji vya loliliondo na sale
ambavyo vimekuwa vimekuwa vikikabiliwa na mgogoro wa ardhi kwa zaidi
ya miaka 20 .
Mkakati huo ambao unatajwa kuwa ulianza mwaka 2009 baada ya serekali
kufanya operesheni ya kuwaondoa wafugaji hao kwa nguvu kutokana na
sababu mbalimbali zilizodaiwa ikiwemo ya uharibufu wa mazingira
,ongezeko la watu hususa ni kutoka katika nchi jirani ya kenya
,kulinda vyanzo vya maji pamoja na ikolojia ya hifadhi ya serengeti.
Aidha mashirika ya kiraia yanayojihusisha na utetezi wa haki za
binadamu na haki za aridhi walibanisha kuwa sababu hizi zote sio za
kweli na kwamba zilikuwa ni hila za kutaka kuwanyang'anya wananchi
ardhi yao ya asili na katika hayo serekali katika kuhalalisha mpango
wa kuwapokonya wananchi wa loliondo ardhi yao walitengeneza mpango wa
matumizi bora ya ardhi mwaka 2010 mpango ambao ulikataliwa na wananchi
kutokana na kuto shirikishwa.
Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa Lashehabingo Charles
Ndangoya alisea kuwa tatizo hili limekuwa la muda mrefu sasa na
katika mwaka wa 2012 serekali iliitisha vyeti vya baadhi ya vijiji vya
loliondo vilivyokuwa vimepimwa kwa madai kuwa vilikuwa na migogoro na
vijiji jirani jambo ambalo sio la kweli huku akibinisha kuwa vijiji
vilivyotajwa kuwa vinamgogoro ambavyo ni ololosokwan na engaresero
vilikataa kurejesha vyeti vyao kutokana na sababu iliotolewa kuwa
hawaoni ukweli wa serekali wenye msingi.
Aliongeza kuwa aikuishia hapo mwaka 2013 serekali ilitaka tena
kuwapokonya wananchi hao eneo hilo la wafugaji wa loliondo kw amanufaa
ya mwekezaji wa kampuni ya uwindaji ya OBC jaribio ambalo wananchi
waliweza kulizuia kwa kutumia nguvu zao wenyewe na wakidai kuwa
ugawaji huo ungeweza kuleta mathara makubwa sana kwa jamii na vizazi
vijavyo ambapo walilazimika kwenda hadi kwa waziri mkuu kupeleka
malalamiko yao ambapo waziri alitoa agizo kwa mkuu wa mkoa kuangalia
namna ya kutatua tatizo hilo ambapo ndipo serekali ilituma tume ya
watu nane kwa ajili ya upimaji ramani wa vijiji vyote vya wilaya ya
loliondo ambavyo havijawai kupimwa ambapo pamoja zoezi hilo lilikuwa
zuri lakini bado walikuwa wanawasisi wasi na pale lilipoanza
kutekelezwa wananchi hao walifurahi wakijua mgogoro wa mda mrefu
umeisha.
Naye mkurugenzi mungine ambaye ametoka katika mashirika hayo ya
utetezi wa haki za binadamu Ambaye ametoka shirika la pingos Forum
Emanuel Siringe yeye alidai kuwa wananchi walifurahia sana swali
wakijua kuwa kile walichokuwa wanatafuta kwa muda mrefu kimepata
umbuzi lakini matumaini hayo yameanza kwisha na kwa sasa hawajui hatma
ya maisha yao kutkana na kile kilichodaiwa mpango wa serekali juu ya
aridhi yao kwani mpango huo ulisitishwa ghafla kwa amri ya waziri wa
ardhi na maendeleo ya makazi bila kueleza sababu ya msingi za
kusitishwa mpango huo wa upimaji.
Aidha alisema kuwa wananchi wamefanya kila juhudi katika kutafuta
ardhi yao na wametumia vyombo mbalimbali kupatza sauti zao ili
serekali isikie lakini haijachukua hatua yeyote na watu zaidi ya
milioni 1.7 wamesini kampeni ilioendeshwa na shirika la kimataifa la
Acaaz kupinga hatua ya rais kikwete kuwaondoa wafugaji wa kimasa
kutoka katika ardhi yao ya asili lakini hawajafanikiwa.
Naye mkurugenzi wa shirika la Ngonet Samwel Nangiria aliomba serekali
kuandaa mpango shirikishi wa kupima vijiji vyote vya loliondo na sale
kama ilivyokusudiwa kufanya hapo awali na kufanya mpango wa matumizi
bora ya ardhi ambayo wananchi ndio wanaamini kuwa ndiyo suluhisho la
mgogoro huu uliodumu kwa uda mrefu,huku akiitaka serekali kuanglia
maslahi ya wananchi zaidi kuliko ya wawekezaji ili kuepuka migogoro
isiyo kuwa na msingi wowote .
"napenda pia kuitaka serekali iache kabisa mpango wake wa kutenga
eneo la kilometa za mraba 1500 kwa maslahi binafsi ya mwekezaji kwani
eneo hilo ni muhimu kwa maisha ya wafugaji wanaoishi loliondo kwa
kizazi cha sasa na kijacho na pia izingatie sana sheria za ardhi za
vijiji katika kushughulikia mgogoro wa loliondo badala ya kuzingatia
sheria za mazingira na wanaya pori pekee"Alisema Nangiria
Habari kutoka Jiachie Blog
0 comments:
Post a Comment