MBUNGE wa Arusha mjini Godbles Lema amewaomba
viongozi wa dini nchini kuwaombea viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) na kuliombea taifa katika kipindi hiki kigumu cha mchakato wa katiba
mpya ambayo imeanza kuleta shida.
Lema alitoa ombi hilo juzi mjini hapa katika
harambee iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Frandis Ksavery Jimbo Kuu
Katoliki Arusha, Parokia ya Olosipa, ambapo alikuwa mgeni rasmi.
“Naomba mtuombee kwani tumedhamiria kuwapigania
wanyonge ndani na nje ya Bunge na hatujali majina yoyote tutakayoitwa kwa kuwa
tunaamini lengo letu ni kuwakomboa Watanzania hivyo kama tutaitwa majina mabaya
kwa lengo hilo basi na tuitwe,” alisema Lema.
Katika Harambee hiyo, jumla ya sh milioni 43,
zilipatikana ambapo Lema na marafiki zake walichangia sh milioni 10.
Fedha hizo zilizopatikana ni sehemu ya sh milioni
120 zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya padri wa kanisa hilo ambaye
hivi sasa anaishi katika nyumba ya kupanga.
Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa harambee
hiyo, Kaimu Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki, Arusha Padri Simoni Tengesi, alisema
mbali ya ujenzi wa nyumba hiyo, kanisa lake lina mpango wa kujishughulisha na
huduma za kijamii ikiwemo ujenzi wa shule, hospitali na huduma nyingine za
wananchi wote bila kujali madhehebu yao.
Chanzo: Tanzania
Daima
0 comments:
Post a Comment