Home » » Wanafunzi wahitimu wa kozi ya uhifadhi wa mazingira wapatiwa kompyuta mkoani Arusha

Wanafunzi wahitimu wa kozi ya uhifadhi wa mazingira wapatiwa kompyuta mkoani Arusha







Na Gladness Mushi wa Fullshangwe- Arusha

WANAFUNZI watatu waliohitimu mafunzo ya kompyuta katika chuo cha uhifadhi wa mazingira   cha
University Times  Training  Insititute kilichoko Moivaro mkoani Arusha
wamepatiwa kompyuta tatu zenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni mbili
ikiwa    ni njia ya kuwawezesha kujiajiri wenyewe baada
ya kuhitimu mafunzo yao.


Wanafunzi hao wamekabidhiwa kompyuta hizo na  mkurugenzi wa chuo hicho Bw Solomon Njiamoja alipokuwa katika hafla  ya mahafali ya
kwanza  ya wahitimu  wa
hoteli management na kompyuta   yaliyofanyika chuoni hapo.


Bw Njiamoja alisema kuwa chuo hicho kimeamua  kuwapa wanafunzi hao kompyuta hizo ili ziweze
kuwasaidia katika kujiajiri wenyewe ambapo wataweza  kukabiliana na hali ngumu ya kimaisha kwa kuwa
vijana wengi wanashindwa kutimiza malengo yao kwa ajli ya kukosa vitendea kazi.

Aidha aliongeza kuwa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi
wanahohitimu chuoni hapo wanapata mafanikio mazuri chuo hicho kinatarajia kutoa
kompyuta 105 kwa mwaka ambapo kila mwanafunzi anayefanya vizuri katika somo
hilo atapata kompyuta yake ya kumuwezesha  kujiajiri.






Mkurugenzi huyo akielezea malengo ya chuo hicho alisema kuwa
kinatarajia kuanzisha redio pia kuanzisha mfuko maalum wa kuendeleza waalimu
kwa kuwa walioko wana shahada ya kwanza hivyo haiwatoshelezi kutoa elimu .

Awali mgeni rasmi katika mahafali hayo diwani wa kata ya  sokoni one Maiko Kivuyo
aliwataka wanafunzi hao kutumia kompyuta hizo vizuri   kwa
kuzitunza na badala yake wasiziuze kwani wako baadhi ya vijana  wakipewa zawadi wanakimbilia kuuza ili wapate
fedha.

Aliwataka vijana hao kutumia elimu hiyo waliyoipata vizuri
kwa kuwa katika dunia ya sasa  hakuna
kitu unachoweza kufanya bila kutumia  kompyuta.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa