Home » » Benki ya posta yawakumbuka wazee wanaoishi katika mazingira magumu

Benki ya posta yawakumbuka wazee wanaoishi katika mazingira magumu




Na.Ashura Mohamed - Arusha
BENKI ya  posta Tanzania imetoa misaada mbali mbali
yenye gharama ya kiasi cha shilingi milioni moja katika kituo cha kuhudumia
wazee wasiojiweza kijulikanacho kwa jina la Sakila Hope for eldery kilichoko
wilayani arumeru mkoani hapa.



Akikabidhi
misaada hiyo kwa wazee hao mkurugenzi mkuu wa benki hiyo bw Saba  saba Moshingi alisema kuwa benki hiyo imeamua
kuungana na wasamaria wema ili kuweza kusaidia kundi hilo kupunguza makali ya
maisha.




Bw Moshingi
alisema kuwa kundi hili la wazee wasiojiweza wamekuwa wakisahulika katika jamii
na kuachiwa wafadhili wenyewe hali ambayo inawafanya nao wajione kuwa
wametengwa na jamii inayowazunguka.

Aliongeza
kuwa kufika kwao katika kituo hicho sio kwa ajili ya zawadi hizo tu bali ni
pamoja na kuwaona wazee hao ili kuyajua mazingira wanayoishi.

Aidha
misaada iliyotolewa na benki hiyo  ni
pamoja na  ,mafuta mchele,unga wa
ugali,sukari,vitunguu,maharage,mafuta ya kula nay a kujipaka pamoja na sabuni
vyote vikiwa na gharama ya milioni moja.

Kwa upande
wake meneja wa kituo hicho bw Amos Baruti  aliiomba serikali kutenga fungu kwa ajili ya
kuwasaidia wazee kwa kuwa wao wamesahulika kutengewa bajeti yao.

“mimi
naiomba serikali iwakumbuke wazee maana wao ndio hazina ya maisha na
wasingekuwa wao hata wengine tusingefika hapa tulipo lakini nashangaa hata
hakuna fungu lao la kuwatunza”alisema Baruti.

Alieleza
kuwa serikali imekuwa ikitenga mafungu kwa ajili ya akina mama na vijana tu na
kuwaacha wazee vijijni huku wakiwa hawana mafungu ya kuwaendeleza kimaisha
hivyo kuiomba serikali kulitupia macho swala hilo

Alisema kuwa shirika hilo linawahudumia
wazee 215 ambao wanahudumiwa katika maeneo ya afya,chakula,malazi burudani
pamoja na kuwapatia huduma za kiroho

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa