Home » » Vyuo vikuu Afrika Mashariki vyatakiwa kufundisha masomo ya biashara

Vyuo vikuu Afrika Mashariki vyatakiwa kufundisha masomo ya biashara



NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA

VYUO
Vikuu Afrika Mashariki vimetakiwa kuwafunduisha wanafunzi wao mafunzo
ya ujasiliamali na masomo yanaoendana na mahitaji ya soko la ajira la
Afrika Mashariki.
Wito huo
ulitolewa na mwenyekiti wa Umoja wa Waajiri Afrika Mashariki, Jackline
Mugo kwenye uzinduzi rasmi wa umoja huo uliofanyika jijini hapa mwishoni
mwa wiki.




Alisema
waajiri wengi katika ukanda wa Afrika mashariki wanakumbana na
changamoto nyingi ikiwemo kutopata wafanyakazi walioiva kwenye maeneo yao ya kazi.



“Hii ni moja
tu ya changamoto nyingi tunazokumbana nazo katika utendaji wetu wa kila
siku kama waajiri na hivyo tunaamini kupitia mwamvuli huu tutaweza kukaa
pamoja kama waajiri na wadau wengine kupata suluhisho la matatizo yetu.” Alisema Mugo.





 “Wanafunzo
wanaomaliza vyuo wanatakiwa kuivishwa vya kutosha kabla ya kuingia
kwenye soko la ajira,” alisema na kuongeza: “Waajiri wanamchango mkubwa
kwenye kuimarisha mtangamano wa Afrika Mashariki kutokana na mchango wao
katika nchi wananchama.”



“Kupitia mwamvuli huu, tunaweza kuishauri serikali juu ya namna ya kuboresha mambo mbalimbali ili kukuza  na kudumisha mtangamano wetu.”



Mwenyekiti wa
Baraza la Mawaziri Afrika Mashariki, Musa Sirma alilipongeza jukwaa la
waajiri kwa kuja na mkakati wao wa namna ya kudumisha mtangamano wa
Afrika Mashariki.



Sirma ambaye ni Waziri wa masuala ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Kenya alisema jukwaa hilo limekuja
katika wakati muafaka ambapo jumuiya inatekeleza itifaki ya soko la
pamoja.



Alisema jumuiya itafanya kila
linalowezekana kuhakikisha kuwa waajiri wanafanya kazi yao katika
mazingira bora na hatmaye kudumisha mtangamano.




Alisema 

waajiri ni sekta muhimu katika jumuiya kwa kuwa wao ni waajiri wakubwa 
wa watu wa Afrika mashariki na kulipa kodi mbalimbali zinazozifanya nchi
zetu kujiendesha.




Umoja huo wa waajiri ulianzishwa mwaka 2010 kwa lengo la kukuza uzalishaji na kuongeza ushindani wa kibishara Afrika Mashariki.
Habari kwa hisani ya Full Shangwe Blog

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa