Home » » WAGONJWA WA MABUSHA WATAKIWA KUNYWA DAWA

WAGONJWA WA MABUSHA WATAKIWA KUNYWA DAWA

NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE BLOG-ARUSHA


IMEBAINIKA kuwa kutokana na baadhi ya wagonjwa wa matende na
mabusha  kuwa na imani potofu ya dawa na
tiba ambzo zinatolewa na wataalamu wa afya imesababisha kuwa na ongezeko la
magonjwa hayo.

Asilimia kubwa ya wagonjwa hao hujenga hofu juu ya madawa
hayo kwa kile kinachosemekana kuwa kuna dawa nyingi sana tofuati na magonjwa
mengine hapa nchini.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa kituo cha afya na utafiti
wa magonjwa ya binadamu(NIMR)Dkt. Mwele Malacele wakati akiongea na wadau wa
utafiti wa magonjwa mbalimbali hapa nchini

Dkt. Mwele alisema kuwa hofu hiyo ya upatikanaji wa dawa
nyingi za mabusha kumesababisha watu kuziogopa sana huku hali hiyo ikisababisha
ongezeko kubwa sana la wagonjwa wa aina hiyo hapa nchini

Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo tayari Taasisi hiyo ya
Utafiti wa magonjwa ya binadamu imeweka mipango mbalimbali ya kuhakikisha kuwa wanawatoa
hofu wagonjwa hao pamoja na jamii kwa kuwa magonjwa hayo ya Mabusha na Matende
yana madhara makubwa sana kwa jamii

“wagonjwa wengi sana wanaogopa hata kutumia dawa za Mabusha
kwa hofu kuwa dawa hizi ni nyingi sana na kwa hali hii inachangia kwa kiwango
kikubwa sana nchi kuwa na wagonjwa wengi ambao ni nguvu kazi ya taifa la
Tanzania”alisema Dkt Mwele

Akiongelea mikakati ambayo imefanywa na Taasisi hiyo hapa
nchini ili kupambana na magonjwa hayo ya Mabusha na Matende Dkt Mwele alisema
kuwa wamejikita zaidi ili kupambana na hali hiyo ambapo kwa sasa watu zaidi ya
Milioni 15 wameshafikiwa na mpango huo wa kudhibiti Matende na Mabusha

Alifafanua kuwa lengo halisi ni kuhakikisha kuwa wanawafikia
wananchi wote wa Tanzania kwa kuwa ugonjwa huo wa Mabusha na Matende una
madhara makubwa sana kwa jamii ikiwemo Umaskini

Aliwataka wananchi wote kuhakikisha kuwa wanaamini zaidi
wataalamu wa afya kwa kuwa imani potofu kama zitaendelea ndani ya Nchi ya
Tanzania ni wazi kuwa umaskini utakithiri kwa kuwa magonjwa hayo yanaweza
kutbitiwa.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa