wanafunzi na walimu kutoka nchini Uholanzi wakikabidhi vifaa vya maabara kwa shule ya sekondari ya oltingi ambayo ni ya kata ya selala wilayani monduli.anayeshuhudia aliyevaa suti nyeusi ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya monduli,Edward Sapunyu.
wanafunzi kutoka nchini Uholanzi wakitoa msaada wa kompyuta ndogo (laptop) kwa wana jumuiya ya shule ya sekondari ya oltinga ambayo ni ya kata ya selela wilayani monduli.
sehemu ya wanafunzi kutoka nchini Uholanzi wakifuatilia shughuli za utoaji wa misaada ya vifaa vya maabara na komputa ndogo kwa shule ya sekondari ya oltinga iliyopo monduli.
baadhi ya wanakiji wa jamii ya kabila la wamasai wakifuatilia upokeaji wa misaada ya vifaa vya maabara na kompyuta ndogo kutoka kwa wanafunzi wa uholanzi.
Novatus Makunga,Arusha
Shule ya sekondari ya kata ya jamii ya wafugaji wa Kimaasai ya Oltinga iliyopo Monduli mkoani Arusha imepata vifaa vya maabara na kompyuta ndogo aina ya laptop kumi na tano vilizotolewa na kundi la wanafunzi na walimu kutoka nchini Uholanzi
Wafadhili hao pia wameahidi kugharamia nusu ya fedha ya uwekaji wa umeme wa nishati ya jua yaani solar power
Wanafunzi hao kumi na wawili na walimu wao wanne wamekabidhi msaada huo katika shule hiyo iliyopo katika kata ya selela ambapo kiongozi wao Marianna Groenewoud ameeleza kuwa wataisaidia shule hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu
Makamu mkuu wa shule hiyo John Masoi ameiomba serikali kusaidia kutoa kiasi kilichobaki cha gharama ya uwekaji wa umeme wa nguvu ya jua unaohitaji jumla ya shilingi milioni kumi na mbili
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli Edward Sapunyu ameeleza kupitia wakala wa nishati vijijini[rea],halmashari hiyo itaweka umeme katika sekondari hiyo
Mratibu wa misaada hiyo kupitia asasi isiyokuwa ya kiserikali ya stichting tanzania support Melchior Nguma ameeleza mbali ya shule hiyo pia wamesaidia shule ya msingi na zahanati ya kijiji cha selela
0 comments:
Post a Comment