Home » » MKUU WA MKOA WA ARUSHA AWATAKA WANANCHI KUTOA TAARIFA SAHIHI KWA WAKATI

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AWATAKA WANANCHI KUTOA TAARIFA SAHIHI KWA WAKATI




Na.Ashura Mohamed -Arusha

MKUU wa mkoa
wa Arusha Magesa Mulongo  amewataka
wananchi wa mkoa huo kutoa taarifa sahihi na kwa wakati katika sensa ya watu na
makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 26 mwaka huu ili kuiwezesha serikali
kurahisisha mpango wa miaka mitano na malengo ya millennia ifikapo 2015.
Mulongo
aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa sensa ya watu na makazi ya
uhamasishaji juu ya maandalizi ya sensa itakayofanyika  nchini kote tarehe 26 agost mwaka huu.
Alisema kuwa
sensa ya watu na makazi ndio chanzo pekee ambacho kinaweza kutoa taarifa sahii
kuhusiana na rasilimali hivyo ni vema wananchi  wakatoa taarifa hizo kwa umakini na weledi  ili serikali iweze kuchukua  hatua za utekelezaji.

Aidha
ameitaka jamii kutowaficha wale wote wenye ulemavu bali wahakikishe kuwa wanatoa
takwimu zao kwa kuwa nao ni watu muhimu katika jamii na wana haki ya kuishi.
“Naombeni
ndugu zangu kundi la walemavu ni watu muhimu sana muhakikishe kuwa mnapata
taarifa zao kwa usahihi kwani wengi wa wananchi huwaficha kwa kudhani ni aibu “alisema
Mulongo

Hata hivyo
aliwataka wasimamizi wa sensa hiyo ambao ni walimu kuhakikisha kuwa wanasimamia
kwa uaminifu na uadilifu na kuacha kutanguliza masilahi mbele.

Kwa upande
wake mratibu wa sensa kwa mkoa wa Arusha Magreth Martin aliwahimiza wadau hao
mambo ya kuzingatia wakati wa kuhamasisha wananchi kuwa ni tarehe ya sensa
pamoja na umuhimu wa sensa kwa jamii kwa kuwa wengi wa wananchi hawatambui
umuimu wake.

Aidha
aliwataka wadau hao kuwaelimisha
wananchi kuwa zoezi la sensa halihusiani kabisa na hofu au imani walizo
nazo na pia wawahakikishie taarifa watakazozitoa wakatii wa kujibu maswali ya
sensa zitakuwa siri na zitatumika kwa maswala ya kitakwimu pekee.

Hata hivyo
hii ni sensa ya tano tangu  kupatikana
kwa uhuru mwaka 1961 na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Ambapo Sensa
ya kwanza ilifanyika mwaka 1967 na kufuatiwa na sensa nyingine za mwaka
1978,1988 na 2002.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa