Home » » WAZIRI WA NISHATI NA MADINI ATAKA WAWEKEZAJI KUJIKITA KWENYE VITO

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI ATAKA WAWEKEZAJI KUJIKITA KWENYE VITO


Ashura Mohamed-Arusha

WAZIRI wa Nishati na Madini, William
Ngeleja amewataka wawekezaji wa madini kuhakikisha  wanajikita zaidi kwenye  ukataji na ung’arishaji wa vito ili kuongeza
thamani ya madini hapa nchini.




Angeleja ameyasema hayo  wakati akifungua maonyesho ya kwanza ya
kimataifa ya madini na vito jijini Arusha yaliyowajumuisha wadau mbalimbali wa
madini wakiwemo wanunuzi wakubwa na wauzaji kutoka ndani na nje ya nchi




Aidha aliwataka wawekezaji kwenye sekta
ya madini kuwekeza kwenye ukataji na ung’arishaji wa madini ili kuongeza ajira
nchini na ukusanyaji kodi hatua itakayoongeza pato la taifa.

Ngeleja ameongeza kuwa  serikali ilizuia usafirishaji nje  wa madini ya tanzanite yasiyoongezewa thamani
ya ukubwa wa gramu moja na kuendelea ili kuwajengea uwezo watanzania waweze
kukata na kung’arisha madini hapa hapa nchini.

Amesema kwa miaka mingi idadi kubwa ya
madini yazalishwayo nchini yamekuwa yakisafirishwa yakiwa ghafi, na
kuisababisha nchi kukosa mapato.

Waziri Ngeleja alisema mwaka jana
serikali ilianzisha utaratibu wa kuhakikisha madini ya Tanzanite yanaonyesha
kuwa yanatoka Tanzania yaani ‘certificate of origin’ kabla ya kuyasafirisha
kuyapeleka nje ya nchi.

 Amefafanua
kuwa serikali inachokitaka ni kufanya  ni
kuhakikisha kuwa  Tanzania inakuwa ndio
kituo cha ununuzi wa madini badala ya kwenda kununua nje ya nchi ,ndio lengo
haswa tunalotarajia kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeweza kuwapatia watu
wengi ajira na kuondokana na umaskini’alisema Ngeleja.

Aliongeza kuwa  hatua hii itasaidia sana kuongeza ajira kwa
watu  na serikali kupata mapato ya
kutosha kutoka kwenye sekta ya madini.

Aliwahakikishia wawekezaji kuwa serikali
itatoa leseni kwa wale watakaojiingiza kwenye eneo hilo na kutambuliwa kama
wawekezaji.

Waziri huyo alisema serikali itaendelea
kusisitiza uwekezaji kwenye uzalishaji wa vito hapa nchini kabla ya kusafirisha
nje.

Alisema hatua hii itawekezekana kutokana
na ushirikiano uliopo baina ya serikali na sekta binafsi ndani na nje ya nchi.

“Tunajitahidi kuwaalika wawekezaji
kutokana na mazingira mazuri yaliyopo,” alisema na kuongeza kuwa Tanzania ina
madini ya aina nyingi ambayo yanatakiwa kuchimbwa.

Maonyesho hayo yameandaliwa na Chama cha
wachimba madini nchini (Tamida), na kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka
nchini na nje ya nchi.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa