Home » » Waandishi wa habari watakiwa kuandika zaidi habari za vijijini

Waandishi wa habari watakiwa kuandika zaidi habari za vijijini

 NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA

WAANDISHI wa habari ndani wa Tanzania
wametakiwa kuhakikisha kuwa wanajiwekea utaratibu wa kuandika habari zaidi za
vijijini kuliko habari za mijini ambapo asilimia kubwa ya wananchi wapo
vijijini na ndipo penye matatizo makubwa sana



Endapo kama vyombo vya habari vitaweza kwenda katika maeneo
ya vijijini kwa wingi basi shida pamoja na kero za wananchi hao wa vijijini
zitaweza kubainika kwa uwazi na kufanya jamii hizo kupatiwa ufumbuzi

Hayo yameelezwa mjini hapa na Bw Saidi Dogoli kutoka UTPC ambaye
alikuwa ni mwenzeshaji wa mafunzo kwa waandishi wa habari za vijijini hasa  kwa mkoa wa Arusha

Bw Dogoli alisema kuwa endapo kama waandishi wa habari
wataweza kuandika na kutangaza changamoto mbalimbali ambayo yanawakabili sana wananchi wa
vijijini  basi ni wazi kuwa wataweza
kupatiwa haki zao za msingi

Alifafanua kuwa kwa sasa asilimia kubwa ya waandishi wa
habari wanaandika habari za mijini wakati kwa upande wa vijijini uadikaji wa
habari ni mdogo sana hali ambayo inachangia kwa
kiwango kikubwa sana
baadhi ya changamoto kuendelea kukua kwenye jamii

“Ni vema kwa wana habari kuhakikisha kuwa wanakwenda zaidi
hasa kwenye vijiji zaidi kuliko hata mijini kwa kuwa kule ndiko kwenye mambo
magumu ambayo yanapaswa kutangazwa na kisha watu kujua umuhimu wa kusaidia
Baadhi ya changamoto”aliongeza bw Dogoli

Awali Waandishi wa habari ambao nao walihudhuria mafunzo
hayo ambayo yalianza juzi na kutarajiwa kuisha kesho walisema kuwa zipo sababu
mbalimbali ambazo zinachanguia kwa kiwango kikubwa sana wao kushindwa kufikia vijijini

Waandishi hao waliongeza kuwa Pamoja na kukabiliwa na
changamoto ya uwezeshwaji  pia wapo
baadhi ya wadau wa vijijini ambao wanashindwa zaidi kuwapa taarifa muhimu na
pia kwa wakati hali ambayo nayo kwa kiwango kikubwa sana  baadhi yao kushindwa kufika.

“Kuna baadhi ya watendaji ambao  hawatoi taarifa kwa wakati kwa visingizio na
hili linakuwa ni kero kwetu lakini hata changamoto nyingine ambayo inatufanya
tushindwe kwenda vijijini ni pamoja na baadhi ya vyombo vya habari kutotoa
kipaumbele kwa habari hizo hali ambayo inafanya wakate tama”walisema
Wanahaabari hao

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa