Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wazee na Watoto Hamis Kigwangalla Akiwa anamtunuku mmoja wa mwanafunzi
wa shahada ya uzamini aliyejulikana kwa jina la Anna
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu
fani za astashahada, shahada ya kwanza
na stashahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii katika chuo cha Taasisi ya
Maendeleo ya Jamii Tenguru wakiwa wanajiself na naibu waziri mara
baada ya mahafali hayo
kumalizika
wanafunzi waliofanya vizuri zaidi shuleni
hapo waliosimama nyuma wakiwa katika picha ya pamoja na naibu waziri
pamoja na bodi ya chuo hicho
Naibu waziri akiongea na waandishi wa
habari mara baada ya mahafali kumalizika wa kwanza kulia
ni Mkuu wa
Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Anatory Bunduki wakwanza kushoto
ni kaimu mwenyekiti wa bodi ya taasisi hiyo Dr,Rosemarie
Mwaipopo
wahitimu wakiwa katika nyuso za
furaha
Na Woinde
Shizza,Arusha
Serikali inajipanga kuajiri maafisa ustawi wa maendeleo ya jamii 5,554 kwakipindi cha miaka mitano ili waweze kutoa huduma za maendeleo ya jamii kuanzia ngazi ya kata na vijiji kama ilivyokuwa kwa utawala wa awamu ya kwanza nchini
Serikali inajipanga kuajiri maafisa ustawi wa maendeleo ya jamii 5,554 kwakipindi cha miaka mitano ili waweze kutoa huduma za maendeleo ya jamii kuanzia ngazi ya kata na vijiji kama ilivyokuwa kwa utawala wa awamu ya kwanza nchini
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Hamis Kigwangalla alipokuwa akihutubia katika mahafali ya sita katika fani za astashahada, shahada ya kwanza na stashahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii katika chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tenguru nje kidogo ya jiji la Arusha
Alisema kuwa serikali ya awamu ya kwanza ilikuwa na idadi
kubwa ya mabibi na mabwana maendeleo ya jamii kila kata hivyo ilisaidia
kuwaletea maendeleo wananchi kwa haraka zaidi na kutoa ushauri wa miradi
mbalimbali inayowazunguka wananchi haswa wa
vijijini.
“katika serikali ya awamu ya kwanza maafisa ustawi wa jamii
walikuwa wapo hadi vijijini unakuta bibi ustawi wa jamii na babu ustawi wa
jamii kitu ambacho kwa kipindi cha nyuma hapa kilipotea kabisa sasa serikali
hii ya awamu ya tano tunataka kurudisha icho kitu”alisema
Kigwangala
Alivitaka vyuo mbalimbali
vinavyofundishia kozi ya ustawi wa jamii kuakikisha wanaongeza idadi ya
wataaalamu wanaosomea
ustawi wa jamii ili
kuweza kupunguaza
tatizo hili kwani kwa sasaivi kadri siku zinavyozidi kwenda ndivo wanafunzi
wanaosomea ustawi wa jamii wanapungua
“ kwasasa wataalamu katika sekta ya
maendeleo ya jamii wameanza kupungua sana na ivyo kila chuo kinatakiwa kuongeza idadi ya
wa wanafunzi ili
kuendana na azima ya serikali
ya kuwa na wataalamu wa maendeleo ya jamii
kila wilaya , kata na hata kijiji.
Kigwangala alitoa wito kwa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kuendela kutoa elimu yenye viwango bora na wazingatie katika mchakato wote wa utoaji mafunzo kuanzia kwenye udahili wa wanafunzi wenye sifa na vigezo ili kujenga jamii ya wasomi wenye tija katika Taifa letu.
" napia napenda
kusema kuwa hao wamaafisa ustawi wa jamii wasome kabisa wakijua
serikali itawaajiri sawa lakini wasitegemee watakaa ofisini tu au
katika ofisi za halmashauri apana wajue kabisa wataenda kufanya kazi
vijijini ili waweze kutambua matatizo ya wananchi na kuyatatua pamoja
nakuvumbua miradi mbalimbali ya jamii itakayosaidia wananchi "alisema
Kigwangala
Alisema Nchi itabadilika sana
na kuwa na maendeleo ikiwa wanataaluma wa Nchi hii wataipenda Nchi yao kama
ambavyo kila mtu ampendavyo mama yake nakujituma sana katika utendaji kazi
utaendana na falsafa ya hapa kazi tu.
Kwa upande wake Mkuu wa Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Anatory Bunduki akisoma hutuba wakati Mahafari hayo alisema kuwa pamoja na mikakati iliyopo ya kuboresha chuo hicho kwasasa chuo kimeanzisha kituo cha taifa cha utafiti na uhifadhi wa machapisho ya wanawake Nchini kituo ambacho kimeanzishwa kwa ushirikiano wa UNESCO na UNFPA pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Kwa upande wake Mkuu wa Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Anatory Bunduki akisoma hutuba wakati Mahafari hayo alisema kuwa pamoja na mikakati iliyopo ya kuboresha chuo hicho kwasasa chuo kimeanzisha kituo cha taifa cha utafiti na uhifadhi wa machapisho ya wanawake Nchini kituo ambacho kimeanzishwa kwa ushirikiano wa UNESCO na UNFPA pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ni kufanya
tafiti za kina kwa masuala ya wanawake, jinsia, watoto wa kike ili kuwainua
kiuchumi, kisiasa,kiutamaduni na kijamii na kuzitumia tafiti hizi kujadili
katika kuandaa sera na kutoa maamuzi yanayojumuisha amsuala ya kijinsia katika
kutekeleza sera mbalimbali hapa Nchini.
Wakwanza kushoto ni mkuu wa taasisi ya
maendeleo ya jamii Tengeru Anatory Bunduki akiteta
jambo na Naibu waziri
Kigwangala
maandamano yakiwa yanaingia katika eneo la shule kwa ajili ya mahafali
baadhi ya walimu wakiwa katika maandamano hayo
0 comments:
Post a Comment