Makamu wa
Rais,Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo ya malighafi inayotumika
katika kutengenezea mafuta yatokanayo na alizeti katika kiwanda cha Mt.
Meru Millers, jijini Arusha.
Makamu wa
Rais,Samia Suhulu Hassan akiangalia moja ya kifungashio cha mafuta ya
alizeti kilichotengenezwa na kiwanda cha Mt,Meru Millers,Arusha.
Makamu wa
Rais,Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi
mbalimbali wa Mkoa na wafanyakazi wa kiwanda cha Mt.Meru Millers,jijini
Arusha.
Makamu wa Rais,Samia Suluhu
Hassani ametembelea kiwanda cha Mt. Meru Millers Limited cha jijini
Arusha kinachojishughulisha na utengenezaji wa mafuta yatokanayo na
alizeti.
Akizungumza baada yakujionea
uzalishaji wakiwanda hicho,amesema lengo kubwa ya ziara yake katika
kiwanda hicho ilikuwa nikujionea shughuli zinazofanywa na kiwanda hicho.
Pia ameweza kusikiliza
changamoto mbalimbali zinazozikabili kiwanda hicho na kubwa ikiwa ni
utozwaji wa kadi nyingi na serikali itahakikisha kunakuwa na utaratibu
mzuri wa ulipaji wa kodi hizo.
Aidha alisisitiza zaidi kuwa
serikali ya awamu wa tano imedhamilia ujenzi wa viwanda vingi nchini
ambavyo vitatumia malighafi za ndani ya nchi nakukuza uzalisha kwa
wakulima na hata pia kutoa ajira za kutosha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mt.
Meru Millers Atul Mittal alisema ikiwa serikali itapunguza kodi hizi
nyingi itasaidia ukuwaji wa viwanda vilivyopo na hata kuhamasisha
wawekezaji wengine kuwekeza kwenye viwanda hapa nchini.
Makamu wa Rais
yupo Mkoa Arusha kikazi kwa mda wa siku 3 ambapo atendelea kutembelea
viwanda vya mkoani hapa na pia atazindua jengo la Mahakama ya Afrika.
0 comments:
Post a Comment