mmoja wa wanakikundicha Marafiki wa Batuli aliyejulikana kwa jina la
Tausi Swalehe akiwa anakabidhi anagawa peniseli kwa baadhi ya wanafunzi
ambao ni yatima wanaosoma katika shule ya msingi Ngarenaro ilipo katika
kata ya Sokoni one ndani ya jiji la Arusha
wanakikundi wa kikundi cha marafiki wa batuli wakiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wanafunzi waliowagawia msaada wa sare za shule
,penseli ,madaftari na kalamu ikiwa ni moja ya mchango wao kama wao
wanakikundi .
Na Woinde Shizza Arusha
Wazazi na watanzania wameaswa kujenga moyo Wa kujitolea kwa makundi maalumu yasiojiweza nakuwapa kile mungu alichowajaalia nakuondoa ubaguzi kwa watoto yatima waliochiwa na ndugu zao.
Wazazi na watanzania wameaswa kujenga moyo Wa kujitolea kwa makundi maalumu yasiojiweza nakuwapa kile mungu alichowajaalia nakuondoa ubaguzi kwa watoto yatima waliochiwa na ndugu zao.
Hayo yalisemwa na Tausi swalehe baada ya kikundi cha
marafiki Wa batuli kufika kutoa msaada kwenye shule za unga ltd,na Sahel
zilizopo kata ya Sokon 1 jijini Arusha nakuwata jamii kuwa na moyo huo
wa kusaidia yatima na makundi yasiojiweza.
Alisema kuwa msaada waliotoa unathamani ya tsh.700,000
vikiwemo madaftari'sare za shule,penseli na pen ambazo zitawapunguzia
adha watoto wenye uhitaji wakiwemo yatima na wasiojiweza ambao
wameshindwa kujihudumia na kufikia malengo.
Alisema kuwa ni vizuri kwa jamii kuendelea kuzijali familia
zisizojiweza na mayatima iliwaweze kufikia malengo yao yakupata elimu
itayowasaidia kujikwamua kimaisha na kuondokana na utegemezi.
''Sio wote wenye kuweza kujiendesha kimaisha yatupasa kama
jamii kujipanga nakuweza kuwasaidia wenye uhitaji natusingoje kuiachia
serikali pekee''alisema Tausi.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya wanafunzi hao wenye
uhitaji mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Unga Ltd Rachel Mussa alisema
kuwa wapo wengi katika jamii wenye fedha lakini wamekuwa hawatumii
vipato vyao katika kusaidia makundi yenye uhitaji.
Akatoa rai kwa makampuni na wenye kuguswa kuweza kujitolea
kwa kile kidogo mungu alichowajaalia kwani wapo watoto wenye uhitaji nao
wajitokeza kuwasaidia.
Nae Mwanafunzi mwenye uhitaji kwa niaba ya wenzake 86
Konsolata Michael alisema kuwa wanashukuru sana kwa msaada huo kwani
umukuja wakati muufaka na kuwataka kuendelea kusaidia watoto yatima na
wasiojiweza na mungu awazidishie pale mlipopunguza kwa ajili yetu.
0 comments:
Post a Comment