Arusha
Home » » SBL kuwapatia maji bure wakazi 65,000 wa Temeke, Arusha

SBL kuwapatia maji bure wakazi 65,000 wa Temeke, Arusha




Oktoba 04, 2016 – Takribani wakazi 65,000 wa maeneo ya Temeke mkoani Dar es Salaam na Likamba mkoani Arusha  hivi karibuni wataanza kufurahia  upatikanaji wa  maji safi na salama bure  huduma  ambayop itatolewa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).
Kwa mujibu wa taarifa  iliyotolewa kwa vyombo vya habari  jijini Dar es salaam leo SBL imesema iko mbioni kujenga na kukabidhi miradi miwili ya maji  katika maeneo ya Likamba na Temeke  kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 170 ili kupunguza  changamoto za uhaba wa maji  unaowakabili  wakazi wa maeneo hayo mawili.
Mkurugenzi wa Mahusioano SBL John Wanyancha  amesema katika taaifa hiyo kuwa  miradi hiyo miwili ya maji  ni sehemu ya programu ya kampuni hiyo ya kusaidia jamii  inayojulikana kama Maji kwa Uhai ambayo inalenga kuzipatia jamii  nchini upatikanaji rahisi na wa uhakika wa  maji safi na salama.
Kwa mujibu wa Wanyancha zaidi ya Watanzania milioni moja wameshanufaika na programu hiyo katika kipindi cha miaka minnne iliyopita kupitia miradi ya maji kama hiyo iliyotekelezwa katika mikoa ya Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma.
Mradi wa Maji kwa Uhai  unajumuisha  uchimbaji wa kisima pamoja na mfumo wake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua (sola) na tenki la maji ambapo kiasi cha lita 45,000 za maji huzalishwa kila baada ya saa sita.
“Kwa miaka kadhaa sasa tumeshuhudia maisha ya familia na kaya  yakibadilika  kijamii na kiuchumi kutokana na miradi hii ya maji  hususani wasichana na wanawake  ambao hawatumiii tena saa nyingi kutafuta  maji safi.  Badala yake muda huo hivi sasa wanautumia  kuhudhuria shule pamoja na kufanya shughuli nyingine muhimu za uzalishaji,” alisema mkurugenzi huyo.
Mkakati wa kusaidia jamii wa SBL pia unalenga  kutoa msaada kielemu  kwa watoto wanaotoka katika familia  maskini, uhifadhi wa mazingira, kuhamasisha unywaji wa pombe kistaarabu na kuwasaidia wakulima wa ndani kwa kuwapatia msaada wa kiufundi na kifedha  ambayo hadi sasa imewasaidia  wakulima nchini  kwa kuboresha maisha yao na maisha ya jamii.
Mwisho

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa