Mkuu
wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo, amewasimamisha kazi watumishi
watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa tuhuma za ubadhilifu
wa fedha za uchaguzi wa mwaka 2015.
Baadhi
ya watumishi wa Halmashauri ya Ngorongoro, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa
Mrisho Gambo(hayupo pichani),alipokuwa akitoa taarifa ya kamati ya
uchunguzi aliyoiunda kuchunguza mapato na matumizi katika halmashauri
hiyo.
Watumishi hao ni pamoja na Bi. Hadija Mkumbwa ambae alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa mwaka 2015 na kumfuta cheo hicho,bwana Evansi Mwalukasa alikuwa mwekahazina wa halmashauri na bwana Sembeli Sinayo yeye alikuwa mwanasheria wa halmashauri.
Maamuzi hayo yamefikia baada yakubainika kuna upotevu wa fedha za uchagu takribani Milioni 188 ambazo matumizi yake hayakuwekwa wazi na pia Milioni 20 zilitumika kwa manunuzi ambayo hayakufuata taratibu za manunuzi ya serikali.
“Kuanzi sasa nawasimamisha kazi
hawa watumishi watatu kwasababu wameisababishia serikali hasara ya
takribani Milioni 128 ambazo zilikuwa fedha za uchaguzi”.
Aidha
Muheshimiwa Gambo alisema maamuzi hayo yametokana na taarifa
aliyokabidhiwa na kamati aliyoiunda yakuchunguza mapato na matumizi ya
fedha za halmashauri hiyo na kubaini upotevu huo wa fedha nyingi ambazo
zingeweza kusaidia shughuli mbalimbali za uchaguzi katika Wilaya hiyo.
Ambapo
fedha nyingine zimetumika kwenye manunuzi ambayo hayakufuata taratibu
na sheria za manunuzi ya serikali ,hivyo ni kinyume kabisa na taratibu
za serikali katika maswala ya manunuzi.
Akisisitiza
kwa watumishi wa serikali kufuata taratibu, sheria na kanuni mbalimbali
katika kutekeleza majukumu yao ili kuepuka migongano na uvunjifu wa
sheria mahala pa kazi nakupelekea kupoteza kazi zao.
0 comments:
Post a Comment