Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo achangia mabati 200 kwaajili ya ujenzi
wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha kijiji cha Engaresoro.
Baadhi
wa wananchi wa kijiji cha Engaresero,wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Arusha,Mrisho Gambo (hayupo pichani),alipofanya ziara katika kijiji
hicho.
Kutokana na changamoto nyingi zinazoikumba sekta ya afya hususani kwenye Zahanati na Vituo vya afya mbalimbali hapa nchini ndio vinapelekea kuwa na huduma duni za kiafya.
“Mimi
nitachangia mabati 200 kwaajili ya ujenzi wa chumba hicho cha upasuaji
na ninaomba wananchi mjitokeze kwa wingi katika ujenzi wa chumba hicho
ili tuweze kunusulu maisha ya kinamama na watoto wanaozaliwa”.
Ukosefu
wa vitendea kazi,upungufu wa watumishi wa afya na ukosefu wa chumba
chakujifungulia ndio changamoto zilizotolewa na wakazi wa kijiji cha
Engaresero Wilayani Ngorongoro.
Akitoa
malalamiko hayo Bi.Omega Lemra alisema wakinamama wengi wanapata shida
sana wanapoenda kujifungua katika kituo cha afya cha Engaresero
kwasababu hakuna chumba cha upasuaji kwa wale wamama wanaojifungua kwa
upasuaji.
“Tumekuwa
tukipata sana shida wakinamama ambao tunaitaji kujifungua kwa upasuaji
kwenye kituo chetu cha afya kwasababu hakuna chumba cha upasuaji na
hivyo kutulazimu kwenda Wilaya ya karibu ya Karatu ambapo pia kuna
umbali”,alisema Omega.
Aidha Gambo amewasisikitiza wananchi wa Engaresero kuchangia mfuko wa bima ya afya(CHF) ilizipatikane fedha kwaajili yakununua vifaa tiba katika kituo hicho cha afya.
Akifafanua
zaidi juu ya upungufu wa watumishi wa afya Mganga Mkuu wa Mkoa,Dokta
Frida Mokiti,alisema halmashauri ya Ngorongoro ipeleke maombi ya
watumishi wa afya wanaoitajika katika kituo hicho nakuwaweka katika
bajeti ili waweze kuajiriwa mapema iwezekanavyo.
Muheshiwa Gambo yupo katika ziara Wilayani Ngorongoro,ambapo
anakutana na wananchi wa vijiji mbalimbali nakusikiliza matatizo huku
mangine yakipatiwa ufumbuzi na mengine yakichukuliwa kwaufuatiliaji
zaidi.
0 comments:
Post a Comment