Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo amepokea mifuko 500 ya simenti
na mabati 500 kutoka kwa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu
kutoka Korea inayojenga barabara ya Tengeru Sakina.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akitoa shukrani kwa kampuni ya
ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu kwa kutoa msaada wa mifuko ya simenti 500
na mabati ya 500 kwa shughuli za maendeleo za Mkoa wa Arusha.
Msaada
huo umetolewa ofisini kwake ambapo tukio hilo limeweza kushuhudiwa na
viongozi mbalimbali wa Mkoa,Wilaya na Wabunge wa viti maalumu wa Mkoa wa
Arusha.
Akipokea
msaada huo,Mrisho Gambo amesema atagawa mifuko 100 ya simenti na mabati
100 kwaajili ya ujenzi wa Zahanati kata ya Murieti kwasababu kumekuwa
na ongezeko kubwa sana la wagonjwa katika hospitali ya Mkoa Mt.Meru
wanaotoka maeneo hayo hivyo ujenzi huo utasaidia kupunguza wagonjwa katika hospitali hiyo.
Pia
yatakayo baki atayapeleka Wilaya ya Longido katika kusaidia ujenzi wa
bweni la shule ya sekondari Longido ambayo liliungua moto nakuteketeza
kila kitu.
“Napenda
kuishukuru na kuipotengeza kampuni ya ukandarasi ya barabara ya Tengure
Sakina na ile ya njia mbadala(by path) kwakutoa msaada huu na kwakuwa
tumeshaanza mkakati
wa ujenzi wa madara kwa shule za msingi na Sekondari,hivyo nitagawa
hayo mifuko ya simenti 100 na mabati 100 ikajenge Zahanati kata ya
Murieti na yaliyobaki yataenda Longido katika ujenzi wa bweni
lililoungua”.
Mkurugenzi Mtendaji
wa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu bwana Xie Jianbao amesema
kampuni yao imetoa msaada huo ikiwa ni moja ya shughuli zao zakusaidia
jamii katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
“Tumetoa
mifuko ya simenti 500 na mabati 500 kama moja ya mchango wetu katika
kusaidia jamii yetu kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo”.
Aidha Mkurungezi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia alisema kutokana
na wingi wa wananchi waliopo katika kata ya Murieti Zahanati hiyo
itaenda kuwasaidia sana na kwakipindi kisichozidi miezi 2 Zahanati hiyo
itakamilika na wananchi wataweza kuitumia.
Ukosefu
wa kituo cha afya katika kata ya Muriet ulibainika baada ya Mkuu wa
Mkoa Gambo kufanya ziara katika kata hiyo nakupata malalamiko kutoka kwa
wananchi kuwa wanatembe umbali mrefu sana kutafuata huduma za afya.
0 comments:
Post a Comment