Wajumbe wa bodi ya barabara ya Mkoa wa Arusha waliohudhulia kikao cha 38 cha bodi hio,jijini Arusha.
Rais
Dkt John Pombe Magufuli ameandika historia kwa wananchi tangu Tanzania
ipate uhuru na kuelekea kutimize mwaka 1 madarakani kwa kuipatia Wilaya
ya Ngorongoro barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 60 tangu Wilaya
hiyo ianzishwe.
Haya yameelezwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakati wa Kikao cha 38 cha bodi ya barabara cha Mkoa huo.
Gambo alisema barabara hiyo inayotarajiwa kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami na itaunganisha mji wa Wasso hadi Sale kilomita 60 imepata Baraka zote kutoka kwa Rais Magufuli.
Gambo
ameeleza katika Kikao hicho kwamba Rais Magufuli ameagiza kuanza
kujengwa kwa barabara hiyo mara moja kwa kiwango cha lami kama
alivyoahidi wakati wa Kampeni alipokuwa katika Wilaya hiyo.
Amesema barabara hiyo inatarajiwa kutekelezwa na Wakala wa barabara mkoani Arusha ( TANROADS).
Mkuu
huyo wa Mkoa amesema hii ni hatua muhimu sana kwa Wananchi wa Wilaya
ya Ngorongoro ,Wilaya haina hata barabara moja yenye kiwango cha lami.
Mkuu
huyo wa Mkoa pia alisema fedha zinazotolewa na wafadhili benki ya
dunia sio msaada bali ni fedha za mkopo kwa Tanzania ambazo Tanzania
italazimika kuzilipa hapo baadaye.
Akitoa
shukrani zake mbunge wa jimbo la Ngorongoro Tate William Ole Nasha
alisema kwa mala ya kwanza Ngorongoro inapata barabara yenye kiwango cha
lami, kweli itakuwa furaha kubwa sana kwa wananchi wa Wilaya hito.
Wilaya
ya Ngorongoro ni kati ya Wilaya sita za Mkoa wa Arusha ambapo Wilaya
hii inakabiliwa na matatizo makubwa ya miundo mbinu ya ukosefu wa
barabara za uhakika ambapo usafiri katika Wilaya hiyo ni wa kubahatisha
kutokana na kukosekana kwa miundo mbinu ya uhakika ya barabara kwenda
maeneo ya vijijini.
Hivi
sasa TANROADS inahudumia kiasi cha kilomita 1,220 katika Wilaya za
Mkoa wa Arusha zikiwemo barabara kuu na barabara za Mkoa alisema Meneja
wa Mkoa Mhandisi John Kalupale.
0 comments:
Post a Comment