Mkuu
wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo ameshiriki ujenzi wa daraja
fupi(drift) katika kijiji cha Orgirah kata ya Mundarara na tarafa ya
Engarenaibow kwa lengo lakuhamasisha wananchi na viongozi wengine.
Akitoa msisitizo kwa viongozi kujitoa sana pale wanapoitajika kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi wao hasa zile ambazo zimeanzishwa kwa nguvu za wananchi wenyewe.
“Viongozi
mbalimbali wasiwe wazito kujitoa katika shughuli kama hizi za maendeleo
ya wananchi na hasa ambazo zimeanzishwa kwa nguvu za wananchi wenyewe
nivema basi na serikali nayo kupitia viongozi kwa ngazi tofauti
kujitokeza nakuunga mkono”.
Mradi
huo wa daraja fupi(drift) ulianza rasmi mnamo Octoba ,2016 kwa lengo
lakuunganisha vijiji viwili vya Orgirah na Igulailungwa ambavyo
vilitenganishwa kwa ukosefu wa daraja hilo fupi na kupelekea kwa vijiji
hivyo kukosa mawasiliano.
Aidha mradi huo mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha shilingi milioni 9 ambapo mpaka sasa ni milioni 6 tu ndio zimetumika katika ujenzi huo, ikiwa Halmashauri ya Wilaya ya Longido ilichangia 450,000, Mkurugenzi wa halmashauri alichangia 640,000 na nguvu za wananchi ni milioni 5.
Hata
hivyo Gambo aliwapongeza wananchi hao kwa juhudi walizozianza za ujenzi
huo na hivyo serikali itawasaidia pale penye mapungufu na wananchi
wenyewe wanatakiwa kujitokeza zaidi hususani kwenye shughuli kama hizo
za maendeleo.
Mradi
huo bado unamapungufu ya shilingi milioni 2 ili kukamilisha milioni 9
kama gharama nzima ya ujenzi na Mkuu wa Mkoa aliaidi kuchangia mifuko 30
ya simenti,pesa taslimu 500,00 na kutoa katapila ikiwa wananchi
watakuwa tayari kuchangia mafuta. Meneja wa TANROAD Arusha Enginia John
Kalupale aliaidi kuchangia mifuko 50 ya simenti.
Pia
mwenyekiti wa chama cha CCM Mkoa Lekule Ole Laiza atachangia mifuko 30
ya simenti, mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido bwana Sabore Molleimet
atachangia 500, 000, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido Juma Muhina nae atachangia 400,000 na Halmashauri yenyewe itaenda kujadili kwenye vikao vyake namna yakusaidia ujenzi huo.
Gambo bado yupo ziarani Longido huku akishirikiana na wananchi wa Wilaya hio katika shughuli mbalimbali za maendeleo yao.
Picha ya pili
Wananchi wa Kijiji cha Orgirah wakishiriki ujenzi wa daraja fupi
(Drift) wakiunga mkono kauli ya Gambo yakushiriki shughuli za maendeleo.
Picha ya tatu
Hili ndilo daraja fupi(Drift) lililojengwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji cha Orgirah, Wilayani Longido.
0 comments:
Post a Comment