Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Meligoi walioikata taarifa ya mtendaji
wa kata yao, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo(hayupo pichani)
katika mkutano wa hadhara, kijiji hapo.
Mkurugenzi halmashauri ya Longido bwana Juma Mohamed Muhina ameamuru kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi mtendaji
wa kata ya Egirai Lumbwa Wilayani Londigo bwana Paulo Luka kwa tuhuma
za ubadhilifu wa fedha za ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Natroni Flamingo.
Maamuzi
hayo yamefikiwa baada ya wananchi wa kijiji cha Meligoi kata ya Egirai
Lumbwa kuikata taarifa iliyosomwa na mtendaji wa kata hiyo iliyoonyesha
ujenzi mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha milioni 50 lakini michango
ya awali ilikuwa milioni 12 na kati ya hiyo milioni 4 tu ndio ilikuwa michango ya wananchi.
Wananchi hao walimweleza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliyekuwa
akisikiliza Changamoto mbalimbali walizonazo baada yakufanya ziara
katika kijiji hicho , walisema kuwa wao wanavyojua wamechanga zaidi ya
fedha zilizotajwa kwenye taarifa hiyo.
Hivyo Gambo alimtaka Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri kufafanua juu ya matumizi ya fedha hizo, akifafanua Bi. Mwajuma
mdaira alisema alifanya ukaguzi na kugundua kuwa fedha zilizokusanywa
kwa njia ya michango ilikuwa milioni 95 na milioni 50 kati ya hizo
zilitumika kwenye marekebisho ya majengo ya shule japo hakukuwa na
mikata yoyote iliyoingiwa kati ya shule na mkandarasi.
Pia
fedha hizo zilitumika bila kutumia stakabadhi za malipo za halmashauri,
na kuna wawekezaji 2 ambao ni Winget Windros Safari walichangia mifuko
200 ya simenti na mingine 200 ilitolewa na Kilomberong Hunting kusaidia
ujenzi lakini mifuko 144 kati ya hiyo iliuzwa na fedha zake hazikujulika
matumizi yake lakini bado anaendelea na ukaguzi zaidi.
Hivyo
kumpelekea Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo kutaka kufahamu hatma ya mtendaji
huyo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri aliyekili kupata taarifa hiyo jana
yake tu na hapo hapo akamuamuru kamanda wa polisi Wilaya kumkamata
mtendaji huyo nakumpeleka kituoni kwa maelezo na upelelezi zaidi juu ya
ubadhilifu huo.
Mkuu
wa Mkoa, Mrisho Gambo yupo katika ziara ya kikazi Wilayani Longido kwa
mda wa siku 5 ilikujionea maendeleo na pia kusiliza Changamoto
mbalimbali za wananchi wa Wilaya hiyo.
0 comments:
Post a Comment