Na Alice Mapunda,Arusha.
Muuguzi Mkuu Mkoa
wa Arusha, Bi.Mwamini Juma Nyakwela, amezindua rasmi mpira wa kiume
(Kondom),unaoitwa ZANA kwa mikoa ya Manyara na Arusha ambayo ipo katika
kifungashio kipya,uzinduzi huo umefanyika katika kituo cha mafunzo ya
afya(CEDHA) Jijini Arusha.
Uzinduzi huo umefanyika baada ya mipira hiyo kuwekwa katika vifungashio vipya na hivyo kubadili muonekano uliokuwa umezoeleka zamani.
“Leo
hii tunazindua mipira hii yakiume ambayo imebadilishwa kifungashio
lakini ubora wake uko pale pale,watu endeleeni kuitumia,”amesema.
Watu
wengi waliaacha kutumia mipira hii kwasababu haikuwa kwenye vifungashio
vizuri na wakawa wanatumia aina nyingine ,lakini kwasababu Serikali
inawajali wananchi wake ikaamua kubadili vifungashio ili wananchi
waendelee kuzitumia zaidi.
Kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa zilionyesha asilimia
69 ya wanawake na asilimia 77 ya wanaume wanauelewa mzuri juu ya
matumizi sahihi ya mipira ya kiume lakini ni asilimia 27 tu ndio
wametumia mipira hii.
Aidha
Kaimu Mkuu wa kitengo cha Elimu,Habari na Mawasiliano kwa mpango
waTaifa wa kudhibiti UKIMWI kutoka Wizara ya fya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Edda Katikiro,amesema mipira hii ya
jina la ZANA imeshasambazwa rasmi kuanzia Juni 2016 na zilitengenezwa takribani Milioni 21 lakini bado Wizara inaendelea kutengeneza nyingine zaidi.
Akisisitiza
zaidi juu ya mipira hii yenye vifungashio vipya,amesema wananchi
hawanabudi sasa watumie hii mipira kwasababu hakuna kilichobadilika
zaidi ya kifungashio tu, na Serikali inatoa bure kwa nchi nzima.
“Hii
ni ileile mipira ya kiume iliyokuwa inatumika tokea zamani mabadiliko
haya ya vifungashio yasiwaogopeshe watu wakajua ni mipira
mipya,”alisisitiza Edda.
Kutokana
na dhana potofu iliyokuwepo katika jamii juu ya muonekana ambao haukuwa
mzuri kwa hii mipira ya kiume hususani huko nyuma ikapalekea watu wengi
kutoziamini kwa ubora wake na hata wengine kutozitumia kabisa.
Aidha amewata watu wajitaidi kupata elimu sahihi juu ya matumizi ya mipira hii, ilikupunguza au ikiwezekana kutokomeza kabisa magongwa ya zinaa,UKIMWI na mimba zisizotarajiwa.
Kwa
Mkoa wa Arusha maambukizi ya UKIMWI kwa mwaka 2016 ni asilimia 3.2
kulinganisha ni kiwango cha Taifa cha asilimia 5.1, hivyo kwa Mkoa kasi
ya maambukizi ipo chini,na usambazaji wa mipira ya kiume tayari Mkoa
ulishapeleka maombi yake nakupatiwa mipira hii aina ya ZANA na
imeshasambazwa katika vituo vyote vya afya.
Uzinduzi
kama huu umeshafanyika katika mikoa ya Mbeya na Mwanza na utaendelea
zaidi kwa mikoa mingine na juhudi kubwa imeshawekwa kwa upande wa
Serikali katika kuhakikisha mipira hii inatumika kwa kiasi kikubwa ili
kufikia mwaka 2020 UKIMWI uwe umetokomezwa kabisa na wadau mbalimbali
wazidi kushirikiana na Serikali katika mapambano hayo.
0 comments:
Post a Comment