Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh.Mrisho Gambo akihutubia wageni katika hafla hiyo |
Meza Kuu ambapo wageni rasmi waliketi katika hafla hiyo |
Meneja BRITAM Tanzania tawi la Arusha Bi. Loisi Yatera akizungumza wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo |
Kutoka kushoto ni Mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha Mjini Mh.Felix Mrema, katikati ni Mkurugenzi wa Masoko BRITAM Kenya na mwisho ni Mkurugenzi BRITAM Kenya Bw.Stephen Wandera |
Meneja BRITAM Tanzania tawi la Arusha Bi. Loisi Yatera akiwatambulisha baadhi ya watendaji wa Kampuni hiyo mbele ya wageni waliohudhuria katika hafla hiyo |
Sehemu ya wageni waliohudhuria hafla hiyo katika hoteli ya Mount Meru |
Mbunge wa Arusha Mjini Mh.Godbless Lema pamoja na mke wake wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika hafla hiyo ndani ya Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha |
Mkurugenzi BRITAM Kenya Bw.Stephen Wandera akimsikiliza kwa makini mgeni rasmi wakati akihutubia wageni katika hafla hiyo |
Habari na Woinde Shizza,Arusha.
Kampuni ya Bima ya Britam imeadhimisha miaka 50 ya kutoa huduma za bima nchini Tanzania huku ikiongoza katika utoaji wa huduma bora za bima za magari,nyumba ,mali pamoja na afya.
Sherehe za Maadhimisho hayo zimefanyika katika Hotel ya Mount Meru iliyoko jijini Arusha na kuudhuriwa na Viongozi wa kiserikali pamoja na Wadau wa Bima.
Afisa Mkuu wa Kampuni hiyo nchini Tanzania Stephen Lokonyo amesema kuwa kampuni hiyo imejipanga vizuri kuwahudumia watanzania na kuwafikia watu wengi zaidi ili waweze kunufaika na huduma za bima .
Aliongeza kuwa wao kama kampuni ya bima ya Britam wamejipanga kuwasaidia wananchi mbalimbali wakiwemo wa juu pamoja na wachini kwakuanzisha bima za aina mbalimbali ikiwemo ya mali zao kama nyumba ,bima za afya pamoja bima ya kilimo kwa ajili ya wakulima pamoja na wafugaji.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo aliwataka mashirika ya bima kuwafikiria pia madereva bodaboda kwa kuwaanzishia bima za afya pamoja na bima za vyombo vyao ili pale wanapopata matatizo kama ya kuunguliwa na piki piki zao pamoja na kupata ajali waweze kusaidika kwa uraisi matibabu na kufidiwa pindi wanapopata ajali.
Alisema kuwa kumekuwa na pikipiki nyingi sana hivyo iwapo wataanzisha bima kwa ajili ya pikipiki wataweza kuwasaidia sana vijana pia wataweza kupata wateja wengi waotumia vyombo hivi.
Aidha mkuu huyo wa wilaya alihiasa kampuni ya bima ya Britam pamoja na kampuni zingine za bima kujikita zaidi kwa watu wenye kipato cha chini.
0 comments:
Post a Comment