|
Baadhi ya vijana waliofika katika banda la wizara ya Kilimo na Mifugo wakipata maelezo juu ya ufagaji wa ng'ombe wa kisasa maalumu kwa ajili ya maziwa Dkt John Mpinga kutoka Luti Campus Tengeru |
PICHA NA GADIOLA EMANUEL
Na Dickson Mulashani
Vijana nchini wamehimizwa kushiriki kikamilifu katika
shughuli za kimaendeleo ikiwemo kilimo ikiwa ni sehemu ya kujikwamua na
kuliletea Taifa maendeleo sambamba na kumuunga mkono Rais kwa kauli mbiu yake ya HAPA KAZI TU!.
Hamasa hiyo inadhihirika wazi kupitia kauli mbiu ya maadhimisho
ya siku ya wakulima maarufu zaidi kama
nanenane mwaka 2016 inayosema KILIMO MIFUGO NA UVUVI NI NGUZO YA MAENDELEO,
VIJANA SHIRIKI KIKAMILIFU “HAPA KAZI TU”
ambapo kitaifa yataadhimishwa mkoani Morogoro.
|
Ikiwa ni siku za mwanzo,mwitikio wa wananchi unaonekana kuwa mzuri |
Picha hizi ni kutoka viwanja vya nane nane vilivyopo Njiro
mkoani Arusha .
|
Mkulima wa zao la viazi vitamu akionesha namna viazi vinavyoweza kutengeneza bidhaa zaidi ya moja ikiwemo "tambi" na "crips" |
|
Mboga aina ya kabichi zikiwa katika ubora wa hali ya juu |
|
Hakika kilimo kinapendeza |
|
Afisa wa kampuni inayojishughulisha na utengenezaji wa nishati kwa ajili ya matumizi ya nyumbani akielekeza namna mkaa unaotengenezwa kutumia pumba unavyofanya kazi |
|
Mmoja wa waliotembelea banda la TAHA akiangalia kwa makini zao la Hoho iliyonona vyema ambayo ni sehemu ya mradi wa TAHA |
|
Sehemu ya mabanda ya maonesho yalivyotawala katika viwanja vya nanenane Njiro mkoani Arusha |
|
Wizara ya Maliasili na Utalii nao tayari wamepiga kambi katika viwanja hivyo |
0 comments:
Post a Comment