Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akizungumza na Wakurugenzi na Watendaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika mafunzo kwa bodi za udhamini za mifuko ya hifadhi ya jamii kuhusu uendeshaji na usimamizi wa mifuko ya hifadhi yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mifuko ya hifadhi ya jamii (TSSA) yaliyofanyika jana jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Mifuko ya hifadhi (TSSA) Eliud Sanga akifafanunua jambo katika mafunzo kwa bodi za udhamini za mifuko ya hifadhi ya jamii kuhusu uendeshaji na usimamizi wa mifuko ya hifadhi yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mifuko ya hifadhi ya jamii (TSSA) yaliyofanyika jana jijini Arusha.
Katibu wa Shirikisho la Mifuko ya hifadhi (TSSA) Meshach Bandawe akizungumza katika Mafunzo hayo.
Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama Akitoa cheti kwa Mjumbe wa Bodi ya LAPF Sarah Mwaipopo
Na Pamela Mollel,Arusha.
Waziri wa
Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama ameitaka Mifuko ya
Hifadhi ya jamii kuwekeza kwenye viwanda ili kuchochea uchumi wa viwanda
utakaolisaidia taifa kukua kiuchumi na pia kuwanufaisha wanachama wa mifuko
hiyo kutokana na uwekezaji huo wenye tija.
Jenista
Amesema hayo akizungumza na Wakurugenzi wa Mifuko pamoja na Watendaji katika
mafunzo kwa bodi za udhamini za mifuko ya hifadhi ya jamii kuhusu uendeshaji na
usimamizi wa mifuko ya hifadhi yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mifuko ya
hifadhi ya jamii (ISSA) .
Amewataka
Wakurugenzi hao kuunga mkono Agenda ya taifa ya kulifikisha taifa kwenye uchumi
wa kati kupitia viwanda.
Waziri huyo
amewataka Wakurugenzi wa mifuko kuhakikisha kuwa wanadhibiti mifuko hiyo ili
wanachama waweze kupata mafao yao kwa wakati muafaka bila kuwepo kwa
ucheleweshaji.
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Mifuko ya hifadhi (ISSA) Eliud Sanga amesema kuwa Shirikisho
hilo litaendelea kuhimiza Mifuko hiyo kutimiza wajibu wake katika kutoa mafao
bora kwa wanachama wao pamoja na kubuni mafao mapya ili kuwavutia wanachama.
Sanga
amesema kuwa kwa sasa mifuko hiyo imefungua milango yake wazi kuwapokea
wanachama kutoka sekta ambazo si rasmi ili nao waweze kunufaika na mafao .
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment