Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkoa wa Arusha.
Serikali mkoani humu, imeahidi kuwa itaendelea kutengeneza mazingira mazuri kuvutia wawekezaji katika nyanja mbalimbali.
Akizungumza katika uzinduzi wa kituo cha kuuza mafuta cha Total
kilichopo Makuyuni wilayani Monduli jana, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Francis Miti, alisema serikali
itaendelea
kutoa ushiriakiano wa kutosha kuhakikisha wawekezaji wanavutiwa na kuendelea kuwekeza katika maeneo mbalimbali.
Alisema sera ya nchi ni kuwapokea wawekezaji na kulinda mitaji,
kazi zao na kuhakikisha wanafanya bila kubughudhiwa na mtu ikiwa ni
pamoja na kuhakikisha wanashirikiana vyema na jamii inayowazunguka kwa
kufuata sheria na taratibu ili kuvutia wawekezaji wengine.
Aidha, alisema uwapo wa kituo hicho utatoa huduma kwa wananchi
wengi wakiwamo madereva wa magari ya utalii wanaofanya shughuli zao
katika Hifadhi za Taifa kama vile Manyara na Tarangire, Serengeti na
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).
“Sisi tunashukuru kampuni hii kuja kuwekeza katika eneo hili
ambalo ni njia panda na bidhaa hii ilikuwa tabu sana kuipata katika
maeneo haya hivyo basi wametoa ajira na kuahidi kuendelea kutoa kwa
akina mama katika mgahawa wake hivyo basi ni fursa na nina hakika
wananchi watanufaika na kituo hiki,’’ alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Total Tanzania,Tarik Moufaddal,
alisema kampuni hiyo imejipanga kutoa huduma bora ikiwepo mafuta bora na
kuhudumia wananchi kwa kuchangia maendeleo yao ikiwamo kutoa misaada
mbalimbali katika sekta ya elimu kwa kutoa madawati na kuboresha miundo
mbinu.
Pia alisema kituo hicho mpaka sasa kimetoa ajira za kudumu na za
muda kwa watu 15 hivyo kuisadia serikali kupambana na tatizo sugu la
ajira, ikiwa ni pamoja na kuwauzia wananchi vifaa vya umeme wa jua kwa
bei nafuu ili kuwawezesha wananchi kukabiliana na changamoto ya kukosa
nuru yaani mwanga.
Nao baadhi ya waendesha bodaboda akiwapo Humphrey Zephania, pamoja
na Samwel Mollel, walisama ujio wa kituo hicho kutawawezesha kupata
huduma ya mafuta saa 24 kwa kuwa hapo awali walikuwa wanafuata mafuta
katika
eneo la Mto wa Mbu, Karatu na wakati mwingine Arusha mjini kutokana na kukosa kabisa kituo cha mafuta katika wilaya hiyo.
''Muda mwingine pindi ambapo kunakuwepo na tatizo la umeme tunakosa
kabisa huduma ya mafuta lakini sasa muda mwingi hapa pako wazi hivyo
kutuwezesha kufanya shughuli zetu masaa ishirini na manne bila kujali
umeme upo ama haupo," alisema.
Pia aliiomba serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini kuthibiti
ubora wa mafuta na wakati mwingine kuzuia upandishaji wa bei ya mafuta
kiholela kwa kuwa unawaathiri katika utendaji kazi wao ikiwapo
kuvifungia kabisa vituo hivyo
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment