Wazee wa Kimasai wamuhakikishia Kinana uaminifu wao kwa CCM
Wataka wafugaji wamilikishwe ardhi
Waitaka serikali kuboresha maisha ya wafugaji
Wataka wazawa wapewe kipaumbele zaidi
Watoa salaam kwa Rais ,wampa pole na wamshukuru kwa kutimiza ahadi yake ya kuwapa mifugo.
Wataka wafugaji wamilikishwe ardhi
Waitaka serikali kuboresha maisha ya wafugaji
Wataka wazawa wapewe kipaumbele zaidi
Watoa salaam kwa Rais ,wampa pole na wamshukuru kwa kutimiza ahadi yake ya kuwapa mifugo.
Diwani wa Viti Maalum Ngorongoro Tina Timan akizungumza wakati wa
mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alitaka
mamlaka husika kubadili sheria kandamizi ili jamii ya Wamasai wafaidike
na ardhi yao .
Mwakilishi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Diwani Viti Maalum
Maanda Mgoitiko akichangia mada wakati wa mkutano wa Wawakilishi wa
Mabaraza ya Wazee wa Kimila wa Kimasai na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana
Mzee wa Kimila kutoka Ngorongoro Jerubi Mkati akizungumza wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Lembulung Ole Kosyando kutoka Kiteto akizungumza juu ya migogoro ya
ardhi inayowakabili ambapo alisema viongozi wa kiserikali na wa kisiasa
wanamiliki ardhi kubwa kinyume na taratibu kiasi cha kuleta migongano
mikubwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza kwa makini
pamoja na Mbunge wa Longido Ndugu Michael Lekule Laizer (kushoto) pamoja
na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Onesmo Ole Nangole.
Sarah Yohana akizungumzia namna wanawake wa Kiteto wanavyoishi kwa
mashaka kutokana na maisha yao kuwa hatarini na kuitaka serikali kufanya
juhudi katika kutatua migogoro iliyokithiri Kiteto.
Doroh M. Kipuyo Diwani wa Monduli (Wanawake) akizungumzia jinsi
wamasai wanavyoumia kuona Serikali haichukui hatua za haraka kwenye
matatizo yanayowakabili.
Wazee wa Kimila wa Kimasai wakiandika yale muhimu wakati wa mkutano
na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika Namanga.
Leboi Sumuni kutoka Monduli akielezea namna wamasai walivyo na
mapenzi na Chama Cha Mapinduzi na kutaka Chama hicho kionyeshe mapenzi
kwa wamasai kwa kusaidia kutatua kero zao ambazo zinaonekana kuwa kubwa
siku hadi siku.
Wazee wa Kimila wakifuatilia mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana( kulia) akisikiliza kwa
makini wazee wa kimila wa Kimasai pamoja na Mbunge wa jimbo la Longido
Michael Lekule Laizer ambaye alisaidia kutafsiri baadhi ya hoja
zilizozungumzwa kwa lugha ya kimasai.
Philipo Kiloe Laiser Diwani wa kata ya Lubomba Longido akizungumzia
Wazee wa Kimasai na kuwaelezea kuwa ni watu wenye hekima busara na
wanatambulika kwenye jamii.
Esupat Ngulupa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido akichangia
jambo wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mzee wa Kimila wa Kimasai wakifuatilia kwa makini mkutano huo ambao ni hatua zaidi za kutafuta suluhisho la migogoro yao .
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Onesmo Ole Nangole. akiongea machache kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu kuongea.
Mbunge wa Longido Michael Lekule Laizer akizungumzia masuala mbali
mbali yanayoikabili wamasai na namna ya kuyatatu ikiwa pamoja na
kujengwa kwa viwanda vitakavyodhalisha bidhaa zitokanazo na mifugo.
Mbunge wa Kiteto Benedicto Ole Nangole akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka akichangia mada
wakati wa mkutano wa Wazee wa Kimila wa Kimasai na Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alisema suala zima la ajira liwe kwenye
uwiano wa sura ya nchi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wazee wa
Kimila wa Kimasai na kuahidi kuyafanyia kazi matatizo yanayowakabili kwa
muda mrefu kwa kushirikiana na wabunge wa CCM
Viongozi wakimila wakimsalimia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe la baraza la Wazee wa Kimila mara baada ya kumaliza mkutano.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment