Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana (kulia)
akizungumza katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi
ya jamii unaotarajiwa kumalizika leo jijini Arusha. Katikati ni Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na
kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi Wetu, Arusha
UTIAJI
saini wa mikataba ya kimataifa, inayohusu hifadhi ya jamii kumeiwezesha
Tanzania kuwa katika hatua nzuri ya kutekeleza ajenda yake ya
kuhakikisha kwamba wananchi wake wanakuwa na haki sawa katika kujipatia
maendeleo na ustawi.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto, Dk Pindi Chana katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu
hifadhi ya jamii mjini hapa.
Alisema
mikataba mikubwa ya kimataifa ambayo Bunge la Tanzania limeridhia na
iliyoleta mabadiliko makubwa katika sera na sheria nchini ni pamoja na
Mkataba wa Kufuta Aina zote za Ubaguzi na Unyanyasaji kwa Wanawake
(CEDAW) wa mwaka 1979, Mkataba wa Haki za Watoto (CRC) wa mwaka 1989
na Mkataba wa Afrika wa Haki za Watoto.
Mkurugenzi
mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao makuu ya
UNICEF, Bi. Alexander Yuster, akiibua hoja kwenye mkutano mkubwa wa
kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania
kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana
uzoefu juu ya nini cha kufanya kusaidia makundi maalumu katika jamii
unaomalizika leo jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Kitengo cha
Ushirikiano na Maendeleo kwenye Ubalozi wa Sweden nchini, Maria Van
Berlekom.
Mikataba
mingine ni Mpango wa Maendeleo wa Milenia (MDGs), Azimio la Umoja wa
Mataifa Namba 1325 la mwaka 2000 na Azimio Namba 1820 la 2006, ambayo
inazungumzia ushiriki na uwezeshaji wa wanawake katika kutanzua
migogoro na ujenzi wa taifa.
Alisema
kitendo cha kuridhia kwa mikataba na maazimio hayo, kinaonesha ni kwa
namna gani serikali ina utashi wa utekelezaji wa maazimio hayo kwa lengo
la kuhakikisha watoto na wanawake, wanalindwa dhidi ya vurugu za aina
zozote na kuwanyima haki zao za msingi.
Dk.Chana
alisema kwa kuzingatia ushiriki kuleta katika maendeleo ya nchi,
Tanzania imetayarishwa Dira ya Maendeleo ya 2025 ikiwa na vipengele
vyote vya haki vyenye lengo la kuongeza wigo wa ushiriki wa wanawake.
Aidha,
ili kuhakikisha makundi maalumu yanalindwa, serikali pia imetengeneza
Sera ya Maendeleo ya Watoto ya mwaka 2008, ambayo kwa sasa inapitiwa ili
kuingiza mambo mengine yanayohusu haki za mtoto.
Picha
juu na chini baadhi ya washiriki wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa
hifadhi ya jamii wakiwemo watengeneza sera, watafiti na waendeshaji wa
mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Bangladesh,
Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia,
Sudan Kusini na wenyeji Tanzania unaoendelea jijini Arusha.
Aidha,
ikiwa imejikita kuondoa masuala ya kuondoa udhalilishaji wa kijinsia,
serikali imefanya maamuzi mengi yenye manufaa pamoja na kushirikiana na
wadau binafsi kuboresha maisha ya watanzania.
Alisema
kwamba suala la wanawake na maendeleo, limeingizwa katika mkakati wa
taifa wa kupunguza umaskini. Alisema mwaka jana serikali ilitengeneza
programu ya taifa inayohusu wadau wengi ya miaka mitatu ya kuondokana na
ukatili kwa watoto.
Mkutano
huo unaozungumzia hifadhi, ulifunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Iddi ambaye alisema misingi imara imeshawekwa
kusaidia hifadhi ya jamii kuelekea dira ya taifa ya kuwa na kipato cha
kati ifikapo mwaka 2025.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment