Home » » UNEDP YAIKABIDHI TANZANIA MITAMBO YA KUHUDUMIA MAJOKOFU

UNEDP YAIKABIDHI TANZANIA MITAMBO YA KUHUDUMIA MAJOKOFU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
 
TANZANIA imepokea msaada wa mitambo na vifaa vyenye teknolojia ya kisasa ya kuhudumia majokofu, viyoyozi na mitambo ya kupozea.
Msaada huo ni kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Utekelezaji Mkataba wa Montreal kupitia Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO).
Aidha wakufunzi 35 wa fani za kuhudumia majokofu, viyoyozi na mitambo ya kupozea kutoka vyuo mbalimbali vya ufundi na taasisi zinazofundisha fani hiyo nchini wamepewa mafunzo ya teknolojia za kisasa za upozaji ambazo ni rafiki kwa tabaka la ozoni na mabadiliko ya tabia nchini.
Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Julius Ningu wakati wa kufungua mafunzo ya mafundi wa majokofu na viyoyozi yanayohusu teknolojia mbadala za Upozaji Rafiki kwa Tabaka la Ozoni yaliyowashirikisha mafundi kutoka mikoa mbalimbali.
Ningu alisema msaada huo uliotolewa na mashirika hayo unasaidia kudhibiti matumizi ya kemikali zisizo rafiki kwa binadamu kwani zinahatarisha usalama wa maisha ya mwanadamu kutokana na matumizi yasiyo sahihi.
 Chanzo;Habari Leo

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa