Arusha
Home » » TANZANIA SASA KUZUIA KENYA CHAKULA

TANZANIA SASA KUZUIA KENYA CHAKULA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika,Christopher Chiza.
Serikali  ya Tanzania inatarajia kusainiana na Kenya makubaliano ya kuiuzia mazao ya chakula baada ya kukusanya chakula cha kutosha na ziada.
Aidha, wizara imesema hatua hiyo imelenga kukuza soko la ndani hususan kwa wakulima wa mazao hayo kwani wafanyabiashara watapata fursa ya kuuza chakula nje ya nchi.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano kati ya ujumbe wa serikali ya Tanzania na maofisa wa Kenya wakati wa ziara yake nchini humo Julai 1 mwaka huu.

Chiza alisema kuwa Tanzania imeweza kuzalisha chakula na kufikia asilimia 118 mwaka 2013/14 118 na hadi hivi sasa kuna jumla ya tani 176,062 ya chakula katika maghala  yaliyopo Rukwa, Iringa, Mbeya na Songea, na kufanya ziada ya chakula kuongezeka kwa msimu huu kuliko ile ya mwaka jana.

“Kutokana na mvua kuwa nyingi katika maeneo mbalimbali ya nchi, dalili za kupatikana kwa ongezeko la chakula maradufu kwa mwaka huu, zilionekana,” alisema waziri Chiza.

Alisema jumla ya tani 50 zimekwishauzwa katika taasisi na asasi nchini pamoja na nje ya nchi katika Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa