Mmoja wa watuhumiwa hao akipakiwa kwenye Gari la Polisi tayari kwa Kupelekwa Mahakamani kusikiliza kesi yao.
Watuhumiwa wakiwa kwenye gari ya Polisi.
*******
*******
WATU
17 wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu Mkazi jijini
Arusha, kujibu mashitaka 16 yakiwemo ya kuua kwa kutumia bomu,kutesa
binadamu na kusajili vijana na kuwapeleka nje ya nchi kufanya ugaidi.
Watu
hao walifikishwa mahakamani hapo leo na kusomemewa shitaka hilo mbele
ya Hakimu Mkazi Mustafa Siama ambapo hawakutakiwa kujibu chochote
kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa
kusikiliza kesi hiyo.
Watuhumiwa
hao wanadaiwa kutenda tukio hilo Aprili 13,katika nyumba ya kulala
wageni na baa ya Arusha Night Park iliyopo Mianzini jijini hapa,ambapo
kesi hiyo imeahirishwa hadi juni 11 mwaka huu kwa mtuhumiwa namba moja
na namba nne na watuhumiwa wengine waliobaki kesi yao itatajwa tena juni
12
Katika
tukio hilo la mlipuko huo wa bomu watu 14 walijeruhiwa vibaya katika
maeneo mbalimbali ya miili yao hali iliyopelekea mmoja wa majeruhi hao
aliyefahamika kwa jina la Sudi Ramadhani mkazi wa Kaloleni jijini hapa
kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa
Arusha ya Mount Meru.
Kwa hisani ya Mtaa kwa Mtaa Blog
Kwa hisani ya Mtaa kwa Mtaa Blog
Akizungumza
na waandishi wa habari Makao Makuu ya Polisi Arusha,kabla ya watuhumiwa
hao kufikishwa mahakamani,Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai nchini (DCI)
Isaya Mngulu amesema kuwa mara tu baada ya kutokea kwa tukio hilo,
polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama walianza
upelelezi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.
Ameongeza
kuwa pia siku hiyo hiyo ya tukio hilo la mlipuko wa bomu katika baa ya
Arusha Night Park muda mfupi baadae bomu lingine la aina ileile
liligundulika kutegwa katika baa ya Washington ya jijini hapa ambapo
bomu hilo liliondolewa katika eneo hilo bila kuleta madhara .
"Aidha
baadhi ya watuhumiwa hawa pia walibainika kuwa na mikakati ya
mashambulizaya namna hiikatika maeneo mengine na sehemu mbalimbali hapa
nchini ambazo ni taasisi za Serikali na sehemu zenye mikusanyiko ya
watu,ambapo pia wanajihusisha na uandaaji wa vijana kutoka mikoa
mbalimbali hapa nchini na kuwapeleka nchi za nje ili kujiunga na makundi
ya kiuhalifu"alisema Mkurugenzi huyo wa Mashitaka nchini.
Mkurugenzi
huyo amesema kwamba upelelezi wa matukio haya bado unaendelea ili
kuwakamata watiliwa shaka wenginewaliobaki katika matukio ya milipuko ya
mabomu katika Kanisa Katoliki Olasitna uwanja wa Soweto yaliyotokea
mwaka jana jijini hapa na sehemu nyingine nchini.
Ametoa
wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa
lengo la kuwafichua wahalifu wa ndani na nje wa matukio haya ya
kihalifuna matukio mengine kwa lengo la kuvuruga amani na utulivu wan
chi.
0 comments:
Post a Comment