Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ZAIDI ya wafugaji 300 na wafanyabiashara wa maduka ya dawa za
kilimo na mifugo, wamepatiwa mafunzo ya utumiaji dawa za kutibu mifugo
ya aina mbalimbali na virutubisho vinavyotolewa na Kampuni ya BYTRADE
(T) Ltd.
Akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo wafugaji na wauza
dawa za mifugo, Mkuu wa Idara ya Wanyama wa kampuni hiyo, Dk. Omary
Magoma, alisema mifugo yote inasumbuliwa na maradhi mbalimbali, hivyo
inahitaji dawa za kuikinga na kuitibu.
Magoma pia aliwataka wafugaji wanapoona wanyama wao wanadhohofika
waache kuwapa dawa bila ya kugundua aina ya ugonjwa na kuwashauri
kutumia bidhaa za kampuni hiyo kwani ndiyo suluhu ya magonjwa na
virutubisho kwa wanyama na mimea.
“Kwa mfano dawa hii ya GUT-O-CID ni dawa ya kudhibiti kwa ufanisi
bakteria waenezao magonjwa sumbufu kama Salmonella, E.coli. Pia
inadhibiti uzalishwaji wa gesi ya Ammonia inayosababisha harufu kali
bandani ambayo ni chazo cha mafua kwa wanyama, hasa kuku na nguruwe,”
alisema Dk. Magoma.
Alisema kuwa dawa hiyo ambayo huchanganywa kwenye chakula,
hukilinda dhidi ya maambukizi ya bakteria na fangasi, pia huongeza
ladha ya chakula na kuongeza kuwa kwa sasa wameingiza dawa aina 11
sokoni.
Alizitaja baadhi ya dawa hizo kuwa ni Mult-Aminovet ambayo ina aina
zote za vitamin na Amino Acid huku akibainisha kwamba madini yanaweza
kufidia upungufu katika vyakula vya wanyama na kuboresha kiwango cha
utagaji na ubora wa mayai.
Alisema inaongeza matokeo bora kwa ng’ombe wa maziwa na hutumika
kuondoa msongo wakati wa matibabu chanjo, joto kali na usafirishaji kwa
kuku huku pia akiitaja dawa aina ya Enziver kuwa inaboresha
uyeyushwaji na unyonywaji wa chakula mwilini mwa wanyama na hurahisisha
pia ukuaji kwa kuku na nguruwe.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment