Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ELINURU
MOSES PALLANGYO (52) mkazi wa Meru Arusha,
namba yake ya ushiriki ni MS 01, ni mkulima na mfugaji ana shamba la
ukubwa wa robo tatu ekari, analima ndizi na mboga na kufuga ng’ombe,
mbuzi na kuku.
ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Anajituma na
kazi yake inaonekana, watu kutoka ndani na nje ya nchi, vikundi, mashirika naa
watu binafsi huwenda kujifunza katika darasa lake la kujitolea. Anasema "kwa mwaka ninavuna ndizi mikungu 70, ninapata kilo 336 za nyama za
kuku pamoja na maziwa lita 3780"
MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA
DOROTHY DANIEL PALLANGYO (64) mkazi wa Meru
Arusha, namba yake ya ushiriki ni MS 02 yeye ni mkulima na mfugaji ana shamba
la ukubwa wa ekari 2 na anafuga ng’ombe na mbuzi.
ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu Anafuga kisasa na ana banda bora
la mifugo, pia analima kwa kuotesha kwa kufuata ushauri wa kitaalamu. "nina shamba lenye ukubwa wa ekari 2.
Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 30 na ninapata lita 5,040 za maziwa"
MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA
0 comments:
Post a Comment