Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Usiku
wa April 13 2014 kwenye baa iitwayo ‘Arusha night park’ iliyopo
Mianzini Arusha ambayo siku zote ni miongoni mwa sehemu zinazokua na
mkusanyiko wa watu wengi kuanzia jioni, limerushwa bomu wakati watu
mbalimbali wakitazama mpira.
wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ambae amethibitisha kwamba ni
watu 15 wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.
Anasema
wote wamepelekwa hospitali ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha bomu
hilo ni la kutengenezwa kwa mkono na mpaka sasa hajajulikana
alietekeleza shambulio hilo.
Kwenye maelezo mengine pia amesema hakuna aliepoteza maisha kwenye shambulio
hilo ambalo uchunguzi wa awali umeshatoka, ila baadae itatoka taarifa
rasmi pale uchunguzi kamili utakapokamilika.
Chanzo;Dj sek blog
Chanzo;Dj sek blog
0 comments:
Post a Comment