Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MBUNGE
wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amesema kuna hatari Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kutumia wingi wake kuendelea kuikomoa kambi rasmi ya
upinzani bungeni kwa kuchagua wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki
(EALA) toka vyama vingine endapo hakutakuwa na tafsiri sahihi ya kifungu
cha 50 cha sheria iliyounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mnyika alitoa kauli hiyo juzi wakati akitoa ushahidi mbele ya jopo la
majaji watano wa Mahakama ya Afrika Mashariki (EAJC), wakiongozwa na
Jaji Justice Butasi wanaosikiliza shauri namba 6/2012 lililofunguliwa na
aliyekuwa mgombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Antony Komu
kupitia CHADEMA.
Alieleza ni vema kipengele hicho kikapatiwa tafsiri sahihi, ili
kuepusha hatari hiyo aliyodai alianza kuishuhudia tangu uchaguzi wa
mwaka 2006 wakati huo Chama cha Wananchi (CUF) kikiwa kinaunda kambi
rasmi bungeni, lakini mwakilishi wa chombo hicho muhimu hakutokana na
chama hicho na likajirudia tena kwenye uchaguzi wa mwaka 2012 wakati
CHADEMA ikiunda kambi hiyo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment