SHIRIKA la nyumba la Taifa NHC linatarajia kujenga Nyumba 500 za watu wenye kipato cha chini zinazotarajiwa kujengwa katika eneo la Mateves jijini Arusha,ikiwa ni moja ya mkakati wa shirika hilo kuhakikisha kuwa Watanzania hasa wenye hali duni kiuchumi wanapata makazi bora na ya kisasa kwa gharama nafuu.
Akizungumza jana jijini Arusha Mkurugenzi wa biashara na Maendeleo wa NHC ,David Shambwe katika kikao cha Wizara ya Ardhi,Nyumba na Makazi ya makazi kilichojumuisha Viongozi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, alisema kuwa watashirikiana na mabenki ambayo yanatoa mikopo ya muda mrefu kuanzia miaka 10-15 ili kuwawezesha watu wa hali ya chini kumiliki nyumba hizo kwa mkopo.
Alisema mpango huo unatarajia kuzinduliwa rasmi April mwaka huu na kutekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itajengwa nyumba 200 mradi utakaoanza mwezi ujao huku awamu ya pili ikiwa ni nyumba 300 kwa kushirikisha wawekezaji katika kuteleza mpango huo.
Aidha ameeleza kuwa nyumba hizo 500 kwa wastani nyumba moja inakadiriwa kuuzwa kiasi cha shilingi milioni 30 na kuwataka Watanzania watumie fursa hiyo kujipatia makazi bora na lengo la NHC ni kupanga miji na kuondokana na tatizo la ujenzi holela.
Kwa upande wake Mshauri wa Masuala ya mipango miji kutoka kampuni ya Surbana Urban Group ya nchini Singapole ,Anandan Karukaran ameishauri serikali iweke mipango ya kutawanya shughuli za maendeleo nje ya jiji ili kupunguza msongamano katikati ya miji.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment