Home » » Wassira ahamasisha wananchi kudai daftari la wapiga kura

Wassira ahamasisha wananchi kudai daftari la wapiga kura

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

WATANZANIA wametakiwa kudai haki yao ya kuandaliwa daftari la kudumu la wapiga kura ili chaguzi zinazofanyika kuanzia sasa ziwe huru na halali.
Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha jana na mwanaharakati wa Maendeleo, Lilian Wassira alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara yae katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Wassira alisema ili chaguzi zinazofanyika kwa haki na uhuru, lazima Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ifumue daftari la zamani kwa kuwatoa wasio na sifa na kuwaandikisha wenye sifa.
Pamoja na NEC, amewataka wadau na wanaharakati wa masuala ya haki za binadamu kuwahamasisha Watanzania kuhakikisha wanadai daftari la kupiga kura lenye maboresho kama haki yao ya msingi ili wakubaliwe kupiga kura.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa