Wajumbe
wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi
ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakiwa kwenye mazungumzo ya
awali na Mkuu wa Shule ya Arusha (Madam Kitigwa) baada ya kuwasili
katika shule hiyo kwa lengo la kukutana na Kilabu cha Umoja wa Mataifa
shuleni hapo na kuzungumza na Wanafunzi kuhusiana na agenda mbalimbali
za Umoja huo. Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
kikishirikiana na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) wapo katika
ziara ya kuzitembelea shule zenye na zisizo na Vilabu vya Umoja huo kwa
lengo la kufikisha habari na kazi za Umoja wa Mataifa.
Afisa
Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama
akizungumza na wanafunzi-wananchama wa klabu ya Umoja wa Mataifa katika
Shule ya Msingi Arusha Medium ambapo amewasisitiza juu ya umuhimu wa
kuzifahamu agenda mbalimbali za Umoja Mataifa na nafasi yao katika
kuleta maendeleo chanya kwa jamii.
Mwenyekiti
Taifa wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN)
Bw. Rahim Rajab Nasser akizungumza na vijana wa shule ya msingi Arusha
Medium juu ya umuhimu wa vilabu hivyo na umuhimu wa ushiriki wao kuanzia
shule za msingi mpaka Sekondari na Vyuoni.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama
(katikati) akisisitiza jambo kwa vijana wa shule ya msingi Arusha
Medium. Kulia ni Mkutubi wa Maktaba ya kituo cha Habari cha Umoja wa
Mataifa (UNIC) Bi. Harriet Macha na kushoto Mwenyekiti Taifa wa Vilabu
vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN) Bw. Rahim Rajab
Nasser.
Kobe
mwenye umri sawa na shule ya Msingi Arusha Medium iliyojengwa mwaka
1930 akiwa hai mpaka na kuwa kivutio kwa wageni mbalimbali wanaofika
shuleni hapo ikiwemo Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa
(YUNA/UNCTN).
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama
akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha kuhusiana na umuhimu
wa agenda za malengo ya Milenia (MDG’s) yanayotarajia kufikia tamati
2015 ambapo wao kama vijana wameshauriwa kutilia mkazo utekelezaji wa
malengo hayo ikiwemo Usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa Wanawake,
Upatikanaji wa Huduma bora za uzazi na kupambana na Ukimwi, Malaria na
magonjwa mengine.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha
waliobahatika kushiriki mkutano huo ulioendeshwa na Wajumbe wa kituo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa
Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN).
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama
akisalimiana na Mkuu wa Shule ya USA Academy Bw. Elibariki Malisa mara
baada ya kuwasili shuleni hapo. Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
kikishirikiana na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) wapo katika
ziara ya kuzitembelea shule zenye na zisizo na Vilabu vya Umoja huo kwa
lengo la kufikisha habari na kazi za Umoja wa Mataifa.
Wajumbe
wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi
ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakiwa na mwenyeji wa
msafara wao MC Kalinga wa Arusha wakielekea kukutana na wanafunzi wa USA
Academy.
Mlezi
wa Klabu ya Umoja wa Mataifa katika shule ya USA Academy jijini Arusha
Bw. Emmanuel Bayo akitambulisha msafara Wajumbe wa kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa
Mataifa (YUNA/UNCTN).
Mkutubi
wa Maktaba ya Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Harriet Macha
akitoa ufafanuzi juu ya umuhimu wa kuyasoma na kuyatunza machapisho
mbalimbali yenye habari za Umoja wa Mataifa kwa Wanafunzi wa USA Academy
mara baada ya kutembelea sule hiyo.
Mjumbe
wa Kamati kuu ya Utendaji katika Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa
(YUNA) Bw. Haji Musa H akizungumza na wanafunzi wa shule ya USA Academy
waliojitokeza kuupokea ugeni huo ambapo aliwahimiza umuhimu wa
kuendelea kushiriki shughuli mbalimbali za Umoja Mataifa na Asasi hiyo
kwa ujumla.
Baadhi
ya wanafunzi ambao pia ni wanachama wa klabu cha Umoja wa Mataifa
shuleni hapo wakifurahi na kusikiliza mambo mbalimbali yaliyokuwa
yakizungumzwa juu ya kazi na agenda mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Msafara
wa Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na
wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) kwenye
picha ya pamoja na wanafunzi wanachama wa UN Club USA Academy jijini
Arusha kwenye bustani iliyotengenezwa na klabu hiyo shuleni hapo.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama
akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Katiti mkoani Arusha
ambao wameanzisha na kuendesha kilabu hicho shuleni hapo kujiunga kwa
wingi zaidi kwani kutawawezesha kujifunza shughuli za Umoja wa Mataifa
duniani, kuhusishwa na mashirika mengine ya kimataifa, kushiriki katika
mafunzo mbalimbali, warsha na mikutano ndani na nje ya nchi kama vile
National Model UN, the Eastern Africa Model UN, the Africa Regional
Model UN na mengineyo, ikiwemo kupata nafasi ya kuisaidia jamii zao
kupitia program mbalimbali za kujitolea zitolewazo na YUNA kupitia
UNCTN.
Wajumbe
wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi
ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakishuhudia moja katika
vipaji vingi vya wanafunzi wa klabu ya Umoja wa Mataifa katika shule ya
sekondari Katiti.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya sekondari Katiti wakishuhudia vipaji vya
Sarakasi na michezo kutoka kwa wanafunzi wenzao wa klabu ya UN.
Wajumbe
wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi
ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) pamoja na Mlezi wa UN Klabu
na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Katiti wakiwa kwenye picha ya
pamoja mbele ya mti wa kumbukumbu wa klabu hiyo shuleni hapo.
Msafara
wa Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na
wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN)
wakisalimiana na Mkuu wa Shule ya Sekondari Ilboru ya jijini Arusha Bw.
J. Shulla mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Ilboru ya jijini Arusha Bw. J. Shulla akizungumza na ugeni huo.
Mlezi
wa Klabu ya UN shule ya Sekondari Ilboru Mwl. Rashid Killasa akitoa
utangulizi wa ripoti ya maendeleo ya Klabu hiyo mbele ya wanafunzi na
ugeni kutoka Umoja wa Mataifa.
Mwenyekiti
wa Klabu ya Umoja wa Mataifa Ilboru Sekondari Bw. Kamana Msumi
akisisitiza kwa wananchama wape juu ya umuhimu wa kuyashika yale
yaliyoletwa na msafara huo shuleni hapo.
Mjumbe
wa Kamati kuu ya Utendaji katika Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa
(YUNA) Bw. Haji Musa H akizunngumza na wanachama wa klabu ya UN shuleni
hapo juu ya faida mbalimbali zipatikanazo ndani ya Asasi hiyo zenye
manufaa kwa maisha yao baada ya shule.
0 comments:
Post a Comment