WATAALAMU wa masuala ya Uhifadhi na Usimamizi wa Wanyamapori kutoka
katika nchi 20, wamekutana mkoani Kilimanjaro katika kongamano la
kujadili mbinu za kukabiliana na changamoto za kupambana na Ujangili
duniani.
Wataalamu hao kutoka katika nchi za Afrika, Ulaya na Amerika wanakutana kuangalia mbinu za kisasa za kukabiliana na hali hiyo ambayo kwa sasa inaonekana kushika kasi katika masoko mengi.
Katika kongamano hilo la siku 5 linalofanyika katika Chuo cha Uhifadhi na Usimamizi wa Wanyamapori (MWEKA), mjini hapa wadau hao walikubaliana kuwepo kwa umuhimu wa kuangalia upya na kubadilisha mitaala ya kufundishia katika vyuo vya wanyamapori kama njia ya kukabiliana na janga hilo duniani kote.
Wakizungumza na Rai kwa nyakati tofauti, baadhi ya wataalamu walisema kuwa kuna haja kwa Serikali, wafanyabiashara na wananchi kuelimishwa juu ya madhara ya kuwakumbatia majangili.
Akizungumzia suala la utoaji wa elimu sahihi, Mkuu wa Chuo cha MWEKA, Dk. Freddy Manongi, alisema kuwa chuo kimeanza mikakati ya kuboresha mitaala inayotumika katika kuandaa maaskari na wataalamu wa uhifadhi wa Wanyamapori kama njia ya kuwaongezea mbinu za kupambana na ujangili nchini.
Dk. Manongi alisema katika uzinduzi wa kongamano hilo la siku tano linaloshirikisha wadau wa hifadhi ya wanyamapori, linashirikisha nchi zaidi ya 20, masuala mbalimbali yamejadiliwa ikiwemo kujifunza changamoto zinazokabili sekta hiyo.
“Katika kutafuta njia muafaka ya kukabiliana na ujangili, hasa ukatili dhidi ya Tembo na Faru, chuo chetu kimeanza mchakato wa kupitia upya mitaala yake katika hilo tunafikiria kuibadilisha ili kutumia mtaalamu wa kisasa.
“Ni wazi tutaweza kutoa mbinu za kisasa kwa wahitimu wetu ambao watapatiwa mafunzo imara na mazuri ya kuweza kukabiliana na majangili hawa,” alisema Dk. Manongi.

CHANZO;MTANZANIA
0 comments:
Post a Comment