Arusha. Polisi mkoani
hapa, imetoa ufafanuzi kuhusu silaha aina ya bastola iliyokuwa ikitumiwa
na mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, Vailet Mathias (37),
aliyepigwa risasi na polisi Octoba 31,mwaka huu kuwa ni mali yake.
Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi wa mkoani
hapa, Liberatus zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na jijini hapa
kuwa, bastola hiyo ni mali ya kigogo mmoja wa Serikali jina
linahifadhiwa.
“Ninachoweza kusema,bastola aliyokuwa nayo huyo
dada ni mali yake halali na aliipata kwa kufuata taratibu zote,” alisema
Kamanda Sabas.
Alisema hata hivyo, polisi mkoani Arusha bado inafanya uchunguzi wa tukio la kupigwa risasi mfanyabiashara huyo.
Vailet mkazi wa Njiro Arusha alipigwa risasi na
polisi katika jengo la Mamlaka ya Kodi ya Mapato (TRA) mkoani hapa, bado
amelazwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi(ICU) katika Hospitali ya
Kilutheri Arusha.
Mfanyabiashara huyo, aliyepigwa risasi Octoba 31,
anadaiwa alitaka kumpiga risasi polisi aliyekuwa lindo kwa kutumia
bastola yake baada ya kutokea sintofahamu ya maegesho ya magari.
Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk Paul Kisanga alisema, hali ya mfanyabiashara huyo inaendelea vizuri.
Awali Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus
Sabas alisema, mfanyabiashara huyo alipigwa risasi baada ya kulazimisha
kuegesha gari hilo, mbele ya lango kuu la kuingia katika Tawi la Benki
ya CRDB.
“Baada ya kutoka benki alikuta gari lake
limetolewa upepo ndipo aliwafuata polisi waliokuwa jirani na lango hilo
na kuanza kusemeshana nao hadi akapigwa risasi baada ya kutoa bastola
yake.”
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment