wameshinikiza Benki Kuu ya Tanzania kuingilia kati ‘wizi’ huo baada ya uongozi wa benki hiyo kudaiwa kutoshughulikia tatizo hilo kama walivyotaraji.
Shilingi bilioni 7.3 zinadaiwa kuibwa katika tawi moja tu la Arusha katika akaunti za wateja mbalimbali katika kipindi cha kati ya mwaka 2010 na 2013, huku baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakidaiwa kuhusika.
Fedha hizo zinadaiwa kuibwa na mtandao wa baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo katika akaunti za wateja kwa kutumia mbinu mbalimbali, zikiwamo za teknolojia ya mawasiliano.
Tayari baadhi ya wateja wanaodai kuibiwa mamilioni hayo wamefungua kesi Mahakama Kuu katika kitengo cha biashara, Kanda ya Arusha baada ya jitihada za kumaliza jambo hilo nje ya mahakama kushindikana.
Mbali na kufungua kesi hiyo, baadhi wamewasilisha malalamiko yao BoT na kati ya hao ni mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, Pendaeli Mollel, anayedai kuibiwa zaidi ya shilingi milioni 700 katika sakata hilo.
Raia Mwema imeiona nyaraka mbalimbali za sakata hilo zinazobainisha kuwa, Mollel ni mmiliki wa akaunti namba 5789633006, 5792261005 na 5789633334 na kati ya hizo, moja ilikuwa ya fedha za kigeni (Dola za Marekani) na nyingine ya fedha za Tanzania.
Kupitia kwa mwanasheria wake, Omar Iddi Omar wa Kampuni ya Law Bridge ya Arusha, Mollel ameiandikia barua Benki Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Usimamizi wa Benki, akikiomba chombo hicho cha usimamizi wa taasisi za fedha kumsaidia namna ya kupata pesa zake.
Katika barua hiyo ya Julai 26 mwaka huu, mwanasheria wake amebainisha kuwa mteja wake katika kipindi cha miezi minne iliyopita aligundua upotevu wa fedha zake katika akaunti zake tatu ambazo ni 5789633006, 5792261005 na 5789633334.
Kwa mujibu wa mwanasheria huyo fedha zinazodaiwa kuibwa au kupotea ni kiasi cha dola za Marekani 361,722.00 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 578 kwa bei ya ubadilishaji fedha katika soko kwa sasa na pia zimepotea shilingi milioni 225 za Tanzania katika moja ya akaunti hizo.
Katika kutia uzito madai yake, Mollel pia amemwandikia barua Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Exim, Yogesh Manek, akimtaka kuingilia kati suala la fedha zake kupotea.
Katika barua hiyo ya Septemba 10 mwaka huu, Mollel anaeleza kuwa menejimenti ya benki hiyo iliahidi kwamba suala lake litapatiwa ufumbuzi wakati wakiendesha uchunguzi wa ndani kufahamu jinsi fedha hizo zilivyopotea au kuibiwa.
Katika mazungumzo yake na gazeti hili, Mollel alithibitisha kuwasilisha malalamiko yake BoT na akasema; “Ni kweli mimi kupitia kwa mwanasheria wangu nimechukua hatua hiyo nikiamini kuwa idara hiyo ya usimamizi wa benki itachukua hatua stahiki ingawa hadi sasa ni miezi miwili bado hatujapewa majibu yanayoridhisha.”
Akielezea jinsi fedha hizo zilivyoibwa, Mollel alisema zimechukuliwa katika akaunti zake kwa njia tofauti kama kwa uhamishaji wa hundi pamoja na utoaji fedha katika mashine za ATM.
Akitoa mfano Mollel anaeleza: “Taarifa ya akaunti yangu namba 5789633334 ambayo ni dola za Marekani zinaonyesha Oktoba 20, mwaka 2010 nilitoa fedha dola 22,650.00 katika akaunti hiyo jambo ambalo si kweli hata kidogo,”
“Hali kama hiyo pia imetokea katika akaunti nyingine mbili za fedha za Tanzania na shilingi milioni 225,000,000 zimepotea,” alidai.
Aliongeza kuwa anashangzwa na taarifa za benki kuonyesha kuwa amekuwa akitoa au kufanya malipo kupitia hundi au mashine za ATM kwani benki hiyo haikuwahi kumpa hundi yoyote au kadi ya ATM na amekuwa akitoa fedha zake kwa kutumia fomu maalumu ya kutoa fedha.
Kwa upande mwanasheria Omar Iddi Omar alithibitisha kuwa ni kweli kwa niaba ya mteja wake ameandika barua ya malalamiko kwenda BoT kwa lengo la kupata haki.
“Ndiyo ni kweli tumechukua uamuzi huo kwa sababu Benki ya Exim wameshindwa kabisa kuonyesha kujali maslahi ya mteja wangu ambaye alikuwa mteja wao, tumewaandikia barua hadi tano lakini hawakujisumbua kujibu zaidi ya kujibiwa barua moja kutoka wakili wao,” alisema.
Wakili Omar alisema wanadhani kwamba ni busara kutumia njia ya kupata fedha hizo kwa kuitumia BoT.
Akizungumzia madai ya mfanyabiashara huyo Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Benki katika Benki Kuu ya Tanzania, Kenedy Nyoni alikiri kupokea malalamiko ya Mollel.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Benki ya Exim, Yogesh Menek, naye amekiri kuwapo kwa malalamiko ya wateja wa benki hiyo wanaodai kuibiwa fedha zao katika Benki ya Exim - tawi la Arusha na suala hilo linafanyiwa uchunguzi wa ndani na maofisa wa benki hiyo.
“Ni kweli nimepokea malalamiko ambayo mteja unayemtaja ameniandikia barua, mimi kama Mwenyekiti wa Bodi nimetoa nafasi kwa menejimenti yetu kushughulikia matatizo hayo kwa kuwa bado yako ndani ya uwezo wao,” alisema na kuongeza kuwa; “fedha za wateja hao zitalipwa tu lakini ni lazima benki hiyo ijiridhishe kuwa ni kweli wateja walipoteza fedha zao na kila mteja awe na nyaraka sahihi zinazoonyesha alihifadhi fedha hizo kwa kufuata taratibu za kibenki.”
“Kwa wale wenye nyaraka wasiwe na wasiwasi fedha zao zitapatikana, benki iko katika hali nzuri kifedha, ukiangalia hesabu zetu tuna trilioni 1.1 hivyo suala la kushindwa kuwalipa wateja hao halipo kabisa ila cha msingi ni wao kuvuta subira wakati benki ikifanya uchunguzi wa suala hilo,” anasema.
CHANZO: RAIA MWEMA

0 comments:
Post a Comment