Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,Bi Magdalena
Mtengu (kushoto) akitoa maelezo ya utangulizi kabla ya ufunguzi wa
warsha ya mafunzo ya wataalamu kuhusu kemikali zinazodumu katika
Mazingira kwa muda mrefu,inayoanza leo mjini Arusha.
Mkurugenzi
wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,Dkt. Julius Ningu
akifungua warsha ya mafunzo ya wataalamu kuhusu kemikali zinazodumu
katika mazingira kwa muda mrefu,iliyoanza rasmi leo mjini Arusha,
kushoto ni Muwezashaji katika warsha hiyo,Profesa Jamidu Katima wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja ya washiriki wa warsha hiyo.Picha na Evelyn Mkokoi, Arusha
======= ====== =======
Nchi
zinazoendelea ikiwemo Tanzania zinakabiliwa na changamoto ya kuongezeka
kwa maeneo yaliyoathirika na kemikali zinazokaa kwa muda mrefu zaidi
ardhini.
Hayo
yamesemwa leo Mjini Arusha na mkurugenzi wa idara ya mazingira kutoka
ofisi ya makamu wa Rais Dkt Julias Ningu, wakati wa ufunguzi wa warsha
ya siku mbili ya mafunzo ya wataalam katika utekeelezaji wa mkataba wa
Stockhom ambao Tanzania ni wanachama.
Dkt.
Ningu amesema kuwa, kutokana na ongezeko la matumizi ya kemikali
zinazohitajika kwa ajili ya shughuli za maendeleo. Changamoto hii
inazidi kuongezeka siku hadi siku kutokana na upungufu wa wataalam wenye
ujuzi na vitendea kazi sahihi kwa ajili ya kusimamia kemikali hizi
hususan mlundikano wa madawa ya kilimo yaliyokwisha muda wake.
Dkt.
Ningu aliongeza kwa kusema kuwa, changamoto nyingine za kimazingira kwa
sasa ni usimamizi wa kemikali hatarishi ikiwamo kemikali zinazodumu
katika mazingira kwa muda mrefu ambapo suala hili linatokana pamoja na
mambo mengine ukosefu wa ujuzi wa kutosha pamoja na miongozo sahihi ya
namna ya usimamizi.
“Hii
inaweza kusababisha hatari ya watu kuathirika kiafya hivyo, ni jambo la
msingi kujenga uwezo wa wataalam wetu katika kusimamaia na kudhibiti
kemikali hizi ili kulinda afya za watu na mazingira, Alisisistiza”.
Mkataba
wa Stockholm ambapo Tanzania ni mwanachama, unazitaka nchi wanachama
kuweka mfumo wa kitaasisi na kisheria katika kusimamia kemikali
zinazodumu katika mazingira kwa muda mrefu, pamoja na kudhibiti madhara
yake kiafya na katika mazingira.
0 comments:
Post a Comment